SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

MATUMIZI YA CONCEALER
Dondoo

MATUMIZI YA CONCEALER 

Concealer ni kipodozi kinacho tumika kufichia madoa, mikunjo na mabaka usoni, ni sawa na Foundation lakini hii ni nzito kidogo,Concealer ina weza kutumika peke yake bila foundation.

Concealer ina patikana katika rangi mbali mbali kutoka zile zinazo waka zaidi (nyeupe) hadi zinazo fifia (nyeusi) ina faa kuchagua kutokana na rangi yako ya ngozi ili usionekane kituko, watu wengi hupenda kuchukua zenye rangi kali zaidi ya rangi za ngozi zao ili kuficha vizuri madoa,mabaka na hata mikunjo usoni. Lakini ni vyema ukachukua ile inayo endana na rangi yako ili upate muonekano wa kiasili zaidi (natural look).

Aina za Concealer

1) Stick Concealer

Hii in patikana katika kikopo kama cha lipstick ila sio lipstick ni Concealer na hupakwa katika ngozi na si mdomoni

w3ll-people-narcissist-foundation-concealer-stick-z

hii hupakwa kila sehemu ya sura yako na ni nzuri uki blend na mkono,paka usoni na kisha uanze kuiblend kwa vidole.  Ni nzuri kuitumia chini ya macho (kwa ajili ya dark cycles), vipele na sehemu yoyote iliyo fifia kama pembeni ya midomo, macho na pua. ni rahisi kuitumia na ukimaliza kuiblend vizuri ina kupa muonekano asilia zaidi.

2) Pencil Concealer

hii ipo kama pencil au wanja.

CoverGirl-Trublend-Fix-Stick-Concealer

hii ina tumika kuchorea sehemu iliyo athirika na una tumia blush kuiblend, pia nayo ni rahisi kuitumia. Inatumika zaidi chini ya macho na katika sehemu zenye chunusi/vipele.

3)Cream Concealer huja katika kikopo kama cha lipbalm lakini pia zipo katika miundo mingine mbali mbali.

mac-well-defined-collection-studio-sculpt-concealer

hii pia hutumia kupakia uso mzima na una weza kupaka ukitumia vidole au brush. Nzuri kutumika chini ya macho au sehemu yoyote iliyo fifia. ni rahisi kutumia hata ukiwa na haraka.

4) Liquid Concealer huja katika muundo wa Lip gloss

concealer_collage1

ni nzuri ukitumia ku blend na Sponge au Brush na si nzuri kuitumia chini ya macho sababu haifuniki vizuri sehemu hizo lakini unaweza kuitumia sehemu nyingine yoyote katika uso na ikakupa matokeo mazuri.

Matumizi ya Concealer

  • Unaweza kutumia kama Foundation
  • Unaweza kuitumia ku Fake fuller Lips
  • utumika kama eye shadow base
  • kupata perfect eye liner

Jifunze vizuri namna ya kutumia Concealer kwenye video hapo chini

 

Related posts

1 Comment

  1. see here

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/matumizi-ya-concealer/ […]

Leave a Reply