SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Matumizi Ya Maganda Ya Machungwa Katika Urembo
Urembo

Matumizi Ya Maganda Ya Machungwa Katika Urembo 

1. Maganda ya machungwa kutoa vinyweleo usoni 
Maganda ya machungwa huondoa  vinyweleo usoni Wanawake wengi hulala-mikia tatizo la kutokwa na vinyweleo vingi kwenye miili yao. Wengine hutumia mbinu ya kuvinyoa kwa kutumia wembe ambapo badala ya kuvipunguza, husababisha viongezeke na ngozi za nyuso zao kuzeeka. Badala ya kutumia krimu kali au wembe,  maganda ya machungwa yanaweza kukusaidia kuondoa vinyweleo hivyo.

Mahitaji

 • Unga wa maganda ya machungwa au malimao kijiko kimoja. Unaweza kuandaa unga huo kwa kuyakausha maganda hayo juani kwa siku kadhaa kisha ukayatwanga na kuyasaga kupata ungaunga wake.
 • Vijiko viwili vya mafuta ya mzaituni (olive oil)
 • Kijiko kimoja cha unga wa mtama
 • Kijiko kimoja cha maji ya waridi (rose water).

Namna Ya Kuandaa

 • Changanya unga wa maganda ya machungwa au malimao na unga wa mtama kwenye chombo kimoja kisha ongeza mafuta ya mzaituni pamoja na maji ya waridi. Changanya mpaka upate ujiuji mzito.
 • Jipake ujiuji huo usoni na uache ukae kwa dakika kumi. Baada ya hapo, tumia vidole vyako vya mikono kuisugua ngozi yako kwa namna ya kutengeneza mduara, zoezi hilo lidumu kwa dakika tano hadi kumi kisha baada ya hapo, osha uso wako kwa maji safi. Fanya zoezi hilo kila siku kwa kipindi cha wiki mbili hadi tatu, utaona mabadiliko.


2. Maganda ya machungwa kutoa Mba kichwani! Watu wengi wanasumbuliwa na ugonjwa wa mba kichwani, awali nilishawahi kuandika kuhusu tiba nyingine, lakini ninaongeza na hii ili kuwasaidia.
Mara nyingi mba huwa wanatokea nyakati za baridi kwani kichwa huwa ni kikavu sana kama unasumbuliwa na hilo tatizo unatakiwa kuwa makini na mafuta unayotumia na kuhakikisha unatumia mafuta kila unapoosha nywele zako.


Jinsi ya kufanya

 • Chukua chungwa limenye upate maganda yake baada ya hapo chukua limao likamue kisha uweke kwenye Brenda usage upate mchanganyiko mmoja.


Matumizi

 • Osha nywele zako kwanza zitakate na baada ya hapo zikaushe kisha paka mchanganyiko wako kwenye ngozi acha kwa muda wa dakika 20-25 kisha osha kwa kutumia shampuu unayotumia ambayo unaamini ni nzuri.
 • Tumia tiba hii kwa wiki mara tatu utaona jinsi utakavyokomesha moja kwa moja tatizo la mba kichwani.

Jee ulikuwa unafahamu juu ya hili!? 

©binturembo 

Related posts

6 Comments

 1. Click to read

  … [Trackback]

  […] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/matumizi-ya-maganda-ya-machungwa-katika-urembo/ […]

 2. gun shop

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/matumizi-ya-maganda-ya-machungwa-katika-urembo/ […]

 3. weed delivery Toronto

  … [Trackback]

  […] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/matumizi-ya-maganda-ya-machungwa-katika-urembo/ […]

 4. 티비위키

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/matumizi-ya-maganda-ya-machungwa-katika-urembo/ […]

 5. Codeless Automation framework

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/matumizi-ya-maganda-ya-machungwa-katika-urembo/ […]

 6. see this

  … [Trackback]

  […] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/matumizi-ya-maganda-ya-machungwa-katika-urembo/ […]

Comments are closed.