Historia inatuambia kuwa, kwa mara ya kwanza Wanja ulianza kutumika nchini Misri na Mesopotamia zamani ikifahamika kama Ugiriki ambapo watu wake walikua wakipakaa wanja sio tu kwa kujiremba bali pia kujikinga na jua la jangwani. lakini pia wanazuoni wanasema Wanja ulikua ukipakwa kama kinga ya kuepukana na mabalaa (uchawi).
Katika miaka ya 1920 kaburi la Tutankhamun lilikundulika na hapo ndipo wanja ukaanza kutumia katika nchi za ulaya, kama inakumbukwa vizuri miaka hii ya 20 ndipo mabadiliko mengi katika mitindo yalianza kutokea hasa upande wa wanawake, wanawake waliweza kuwa huru zaidi kupaka make up kuliko miaka ya nyuma.
Katika miaka ya mwanzo ya 20 wanja ulikua unatumika sana katika macho na midomo hii ilikua ikiitwa gothic fashion, ambapo lipstick zilikua bado hazija gunduliwa.
staili hii haiku kwa wanawake tu bali hata kwa wanaume pia ambapo wanaume walikua wakitumia kufanya macho yao yavutie zaidi.
Kwa sasa kuna matumizi mbali mbali na aina mbali mbali za wanja (kuanzia rangi mpaka material
Aina za wanja:
- Liquid eye liner – (wanja wa majimaji)- wanja huu una kuja katika ki box kidogo ukiwa na brush yake ya kuchorea ni wanja ambao una tumika sana sasa hivi kwa sababu una leta aina tofauti tofauti za style za kupaka wanja mara nyingi hupakwa juu ya jicho japokua siku hizi una tumika kote kote.
- Wanja wa pencil- huu ni wa mwanzo kabisa yaani wa zamani ambapo zamani ulikua una tumika kwa rangi nyeusi peke yake japo siku hizi zipo rangi nyingi huu upo kama penseli.
- Wanja wa kungu- huu unaweza ukaja katika kibox au hata kama pencil japo huu ni tofauti kidogo husababisha macho kulegea (kurembua), hutumika sana katika kuwaremba ma bibi harusi japo kwa sasa hausikiki sana.
- Wanja wa gel- huu pia una tumika sana siku hizi unakua katika kikopo kidogo na brush yake lakini wenyewe ni laini sana.
Faida za wanja
- Wanja una kinga macho yako dhidi ya jua
- Kuulipa jicho lako muonekano wa tofauti kwa sasa kuna maendeleo makubwa unaweza kutumia wanja kufanya jicho lako kuwa dogo au kubwa.
- Kuupa uso muonekano wa tofauti, wanja ukipakwa kwenye nyusi vizuri basi huupa uso wako muonekano wa tofauti, tofauti na ukiziacha nyusi peke yake.
Matumizi mengine ya wanja
- Unaweza kuutumia wanja kama mascara, endapo utagundua kuwa umesahau kupaka wanja na haupo nao.Unaweza kutumia wanja badala yake.
- Kuweka kidoti cha uongo, kidoti ni moja ya kitu ambacho wanawake wengi wana penda na wana kitumia kama urembo, una weza kutumia wanja kuweka kidoti cha uongo popote upendapo kama pembeni ya mdomo au pembeni ya jicho, lakini kumbuka kuto kukishika shika kitafutika.
3. Unaweza kutumika pia katika kuficha mvi, kama una mvi chache una weza kutumia wanja mweusi kupaka katika zile mvi na kuzificha.
Related posts
1 Comment
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/matumizi-ya-wanja/ […]