SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mchakato Wa Ngozi Kuzeeka Unaanzia Miaka 20
Skin Care

Mchakato Wa Ngozi Kuzeeka Unaanzia Miaka 20 

Makunyazi AU Mikunjo Katika NGOZI Hasa Usoni “facial wrinkles”ni kitendo cha ngozi ya juu ya binadamu kupoteza umbo lake la wali na kuwa dhaifu hivyo kujikunjana kuchora mistari mistari hivyo kufanya ngozi kuwa dhaifu na kupoteza mvuto na uhalisia wake!


Sababu Kuu Ya Makunyazi Ni Kudhoofika  Kwa Collagen Za Ngozi Ambazo Huifanya Ngozi Kuwa Imara Na Afya! Jee Wajua uzee ni Mchakato unaoanzia miaka 20. “aging is a process which starts at 20” . Kudhoofika kwa collagen kunaanzia miaka 20. Na Mchakato huu unaanzia taratibu Sana hadi pale unapoona makunyazi wazi wazi jua uzee unakuingia. Lengo Sio usizeeke Ila uzeeke vizuri “aging gracefully”


Collagen ni nini? 
Collagen ni protini ngumu, isiyoyeyuka na iliyoumbwa kama nyuzinyuzi. Protini hii inayotengenezwa na amino acids hufanya theluthi moja ya protini yote iliyomo ndani ya mwili. Kuna aina nyingi za collagen, kama aina 16 hivi. Collagen hizi za ndani ya mwili ni ngumu sana na aina nyingine za collagen ni ngumu kuliko hata chuma.
Collagen hupatikana zaid kwenye ngozi na mifupa na hufanya kazi ya kuupa mwili uimara na nguvu ikiambatana na elastin. Kwenye tabaka la dermis, collagen hasaidia kujenga mtandao wa nyuzinyuzi unaosaidia seli mpya kukua juu yake. Kwa vile uzalishaji wa collagen mwilini hupungua na umri, ngozi hupoteza hali yake ya kunyumbuka na kuifanya ngozi kubonyea chini. Hivyo, mistari na mikunyanzi hujitokeza.
Kupungua kwa collagen husababisha piaudhaifu wa cartilage kwenye maungio ya mifupa (joints). Collagen huzalishwa na seli mbalimbali lakini haswa na seli za kuunganisha viungo (connective tissue cells). Mwili wa binadamu huendelea kuzalisha collagen vizuri hadi umri wa mtu unapofikia miaka 40 hivi, baada ya hapo uzalishaji hupungua na kuwa kidogo sana umri unapofika miaka 60.


Collagen hutumika kuondoa mistari na mikunyanzi ya juu ya ngozi (kuondoa wrinkles) na pia husaidia kuondoa makovu juu ya ngozi, yale ambayo hayana ncha kali. Collagen inayotumika inatokana na binadamu na wanyama wa jamii ya ng’ombe.


Collagen ni protini ambayo, kama protini nyingine inatengenezwa na amino acids. Kuna amino acids 9 ambazo ni muhimu katika utengenezaji wa collagen na ambazo hupatikana kutokana na chakula tunachokula . Chakula kizuri kwa kutoa collagen ni kile kinachotokana na wanyama, kama vile; jibini, mayai, samaki, maziwa na nyama ya kuku.
Vitu Vinavyosababisha Udhaifu  wa Collagen Na Kuleta Makunyazi1. Jua2.Matumizi Ya Vipodozi Hasa Vyenye Steroids3. Uvutaji wa Sigara4. Msongo wa Mawazo5. Lishe mbovu  6. Kutokunywa Maji Mengi7 Muda Mdogo wa Kulala8. Unywaji wa Pombe Na Mengineyo.

MAMBO HAYO HUSABABISHA MAKUNYANZI HASA USONI KWA HARAKA ZAIDI NDIO KAMA HAYO JUU 

Vitu Ambavyo Hutoa Makunyazi Kwa Haraka Sana

Karoti

Maziwa Mgando

Parachichi

Tango 

Papai

Kiini Cha Yai.

Almond Oil


kuna njia rahisi sana ambazo zina uwezo wa kutatua tatizo la mikunjo bila kuhaha katika maduka ya vipodozi kutafuta losheni au vipodozi ili kukabiliana na tatizo hili. Sasa unaweza kutumia vitu vya kawaida kabisa kuondoa mikunjo kwa urahisi na kuufanya uso wako uonekane kijana zaidi.

  • Baadhi ya njia hizi ni kama;


Kutumia tango,yai na limao

vijiko 2 vya juisi ya matango,

ute mweupe wa yai,

kijiko kimoja cha maji ya limao

  • Maandalizi:

changanya vitu hivyo kwenye chombo kimoja na hakikisha kwamba vitu vyote vimechanganyika sawasawa. Hifadhi mchanganyiko huo tayari kwa kuupaka kwenye uso.

  • Jinsi ya kutumia:

osha uso wako kwa maji na sabuni na hakikisha umeukausha baada ya kuosha uso wakopakaa mchanganyiko wako ulioandaa kwenye uso wako na acha mchanganyiko huo bila kunawa kwa muda wa dakika  15 hadi 20. Kisha osha uso wako kwa kutumia maji ya uvuguvugu Ukitaka matokeo ya kudumu Tumia Anti aging creams na “anti aging skin care routine” utapata kuonekana kijana daima. Zinapatikana sehemu tofauti tofauti Tafuta mtaalamu unaemuamini akusaidie katika hilo. 
Jee Taarifa hii imekusaidia? Shea na uwapendao! 


©binturembo 

Related posts

3 Comments

  1. บาคาร่า

    … [Trackback]

    […] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/mchakato-wa-ngozi-kuzeeka-unaanzia-miaka-20/ […]

  2. แทงหวย

    … [Trackback]

    […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/urembo/mchakato-wa-ngozi-kuzeeka-unaanzia-miaka-20/ […]

  3. Why Buy Cocaine From Crack Dispensary

    … [Trackback]

    […] Read More on to that Topic: afroswagga.com/urembo/mchakato-wa-ngozi-kuzeeka-unaanzia-miaka-20/ […]

Comments are closed.