Kama una dhani muonekano mzuri ni kwa wanawake tu basi unakosea sana, wanaume wana ngozi ngumu za sura kwa sababu ya kunyoa ndevu na kutembea juani, pia hupata chunusi na madoa meusi wakinyoa ndevu lakini hizi ni step nne rahisi za kufuata kuondokana na matatizo hayo,
Osha sura mara kwa mara: kutembea juani husababisha majasho vumbi kuingia katika ngozi pale unapo osha uso mara kwa mara husaidia kuondoa zile vumbi na jasho ambazo zikikaa sana huaribu sura yako kwa chunusi ambazo baadae zinaweza kusababisha madoa usoni, huitaji kemikali osha uso kwa maji masafi tu na utapata matokeo mazuri.
Utaratibu mzuri wa kunyoa ndevu: kwa sababu ukinyoa ndevu huwezi kujifunika uso kwaio ngozi yako inakuwa wazi vumbi huingia kirahisi ni vizuri ukajiwekea ratiba ya kunyoa ndevu usiku au jioni ili ngozi ipate kupumua kwa usiku mzima kabla ya kupigwa na jua, pia baada ya kunyoa tumia vitu vya asili kusafisha uso kama sabuni za muarobaini na kadhalika.
Paka mafuta kulainisha ngozi: wanaume wengi hudhani mafuta ni kwa ajili ya wanawake tu hapana mafuta ni kwa wote paka mafuta katika sura kurainisha ngozi ya uso hasa kutokana na kwamba ngozi hukakamaa kutokana na kupitisha wembe katika kunyoa ndevu.
Nyembe: ni vizuri kama utatumia kiasi kikubwa cha fedha katika nyembe kuliko kutumia nyembe za bei rahisi ambazo zinaweza kusababisha ukakamavu wa ngozi ya uso, miwasho na hata vipele.
Related posts
4 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/mwanaume-fuatisha-haya-kwa-muonekano-mzuri/ […]
… [Trackback]
[…] There you can find 91414 additional Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/mwanaume-fuatisha-haya-kwa-muonekano-mzuri/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/mwanaume-fuatisha-haya-kwa-muonekano-mzuri/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/mwanaume-fuatisha-haya-kwa-muonekano-mzuri/ […]