SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna 3 Za Kutumia Aloe Vera Kuondoa Madoa Katika Ngozi
Urembo

Namna 3 Za Kutumia Aloe Vera Kuondoa Madoa Katika Ngozi 

Weekends ni muda mzuri wa kujijali mwenyewe, kwenda salon kuosha na kusafisha nywele, kujali kucha zako, kupumzika lakini pia ni muda mzuri wa kujali ngozi yako. Week nzima una amka asubuhi na kwenda kazini unatembea juani na kukosa muda wa kujijali ila inapofikia weekend basi inabidi uvijali vile vyote ambavyo hukuweza kufanya.

Leo tumewaletea namna unavyo weza kutumia mmea wa Aloe Vera (m-shubiri) kutibu ngozi yako kwa kuondoa alama nyeusi zilizo takana na chunusi au kuungua na jua. Aloe Vera Ina anthra-quinone ambayo husaidia kuondoa dead skin cells naturally, hii hupelekea kusafisha na kung’aza ngozi na kutibu tatizo lolote la ngozi zikiwepo chunusi na madoa yaliyo tokana na chunusi

Aloe – vera ina faida nyingi katika ngozi na hutibu magonjwa mengi ya ngozi lakini leo tunawaletea njia 3 za namna unaweza kutumia Aloe – Vera kuondoa weusi katika ngozi.

Vitamin E na Aloe Vera Gel ( Ute wa mshubiri/aloe vera)

Mahitaji:

 • Ute wa Aloe Vera – kijiko kimoja
 • Vitamin E – Nusu Kijiko

Namna Ya Kufanya

 • Changanya mahitaji yako kwa pamoja, unaweza kutumia Vitamin E oil au kutumia vidonge kivunje katikati na changanya na ute wa aloe vera mpaka kiyeyuke
 • Safisha uso wako kwa kutumia chochote ambacho unatumiaga kusafishia kila siku na taratibu chukua mchanganyiko wako upake kwenye madoa na uanze ku massage sehemu hio
 • uache mchanganyiko wako ukauke huchukua takribadi dakika 30-35
 • Osha/Safisha sehemu uliyo paka mchanganyiko wako na uache ngozi ipumue.
 • Fanya hivi mara mbili kwa week kupata matokeo bora mapema.

Asali Na Aloe Vera Gel ( Ute Wa Mshubiri/Aloe vera)

Mahitaji 

 • ute wa aloe vera – kijiko kimoja
 • Asali – kijiko kimoja
 • manjano – robo kijiko

Namna Ya Kuandaa

 • Changanya mahitaji yako kwa pamoja
 • Safisha uso wako kwa kutumia chochote ambacho unatumiaga kusafishia kila siku na taratibu chukua mchanganyiko wako upake kwenye madoa na uanze ku massage sehemu hio
 • iache ikauke katika ngozi yako kwa muda wa dakika 20-25
 • safisha uso wako kwa maji ya uvugu vugu na iache ngozi ipumue kwa muda kabla ya kupaka vipodozi vyako.
 • fanya hivi mara mbili kwa week kupata matokeo bora.

Limao/Ndimu na Aloe Vera Gel 

 

Mahitaji:

 • Aloe Vera Gel – vijiko vitatu
 • Ndimu – Kijiko Kimoja
 • Asali – Vijiko Viwili

Namna Ya Kuandaa 

 • Changanya mahitaji yako kwa pamoja
 • Safisha uso wako kwa kutumia chochote ambacho unatumiaga kusafishia kila siku na taratibu chukua mchanganyiko wako upake kwenye madoa na uanze ku massage sehemu hio
 • acha mchanganyiko wako ukae kwa muda mrefu, unaweza kupakaa usiku ukalala nao ukisha kauka. Hii inasaidia sana endapo tu utakaa nayo kwa muda mrefu usoni
 • Osha na ondoa mchanganyiko wako kwa maji ya baridi.
 • Tumia njia hii kila siku kwa matokeo bora.

 

 

Related posts

4 Comments

 1. Air Force 1 Mushrooms – 4 Oz

  … [Trackback]

  […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-3-za-kutumia-aloe-vera-kuondoa-madoa-katika-ngozi/ […]

 2. web cam hairy bbw pussy feet up

  … [Trackback]

  […] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-3-za-kutumia-aloe-vera-kuondoa-madoa-katika-ngozi/ […]

 3. this website

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-3-za-kutumia-aloe-vera-kuondoa-madoa-katika-ngozi/ […]

 4. magic mushroom microdosing amount

  … [Trackback]

  […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-3-za-kutumia-aloe-vera-kuondoa-madoa-katika-ngozi/ […]

Comments are closed.