SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Gani Manukato Yanaweza Kukutambulisha
Urembo

Namna Gani Manukato Yanaweza Kukutambulisha 

Manukato yanauwezo wa kipekee wa kuweka kumbukumbu, kuongeza kujiamini na kuamsha hisia za watu, ingawa watu wengi hufurahia kujumuisha manukato katika shughuli zao za kila siku ila baadhi wanapenda kutumia manukato kulingana na shughuli maalumu. Leo nakupa vidokezo muhimu na mbinu za jinsi ya kutumia manukato mara kwa mara kuhakikisha unazungumza na kila nafsi kupitia harufu yako.


Chagua perfume kulingana na tukio

Zingatia sana matukio ambapo ungependa kufanya muonekano ambao hakuna atakayesahau mfano harusi, dinner dates au mikusanyiko rasmi. Ukiweza kuchagua perfumes zile zinazoweza catch attetion ya kila mtu kwenye matukio hapo ni ngumu kusahaulika kila muda mtu anapofikiria harufu yako.


Chagua manukato ya kudumu

Kwa kuwa utakuwa unatumia manukato mara kwa mara ni muhimu kuchagua manukato ambayo yanakaa muda mrefu, angalia viwango vya manukato au eau de perfumes kwasababu zinakuwa na viwango vya juu vya mafuta na hukaa muda mrefu kwenye ngozi. kuchagua perfumes zinazokaa muda mrefu husaidia kuhakikisha kuwa harufu hio inaendelea kuwepo kwa tukio zima na hivyo kukuwezesha kufurahia hali yake ya kuvutia kwa muda mrefu.


Tumia Perfume kwa usahihi

unapotumia manukato ni muhimu kuyapaka kwa usahihi anza na kunyunyiza kiasi kidogo kwenye sehemu kama vifundo vya mikono, shingo au nyuma ya maskio, maeneo haya huleta joto hivyo husaidia harufu kuenea siku nzima, kumbuka “ Less is more when it comes to perfumes” hivyo epuka kutumia perfume nyingi kupita kiasi hii inaweza kuwakera waliokaribu na wewe.


Tumia bidhaa zinazoendana na perfumes zako

Hii inaongeza kudunu kwa harufu nzuri mwilini, mfano matumizi ya bidhaa kama shower gel na lotions au mafuta ya maji, mbinu hii inaongeza longevity ya manukato mwilini.
Hifadhi perfumes mahali sahihi: manukato yanapaswa kuhifadhiwa mahali pa baridi, pakavu na mbali na jua, ukihifadhi sehemu isiyo sahihi husababisha kubadili harufu yake halisi lakini pia jitahidi kuhifadhi katika packages zake maalumu kuhakikisha usalama wake.


Hivyo matumizi ya manukato mara kwa mara ni njia bora sana ya kutengeneza memories mara zote unapokutana na watu usidanganyike kunukia raha sana. So “Embrace the art of Occassional perfuming and let your unique scent tell a captivating story.

Imeandikwa na @this_is_lydia._

Sponsored By @EMATScents

Related posts