SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Nyingine Za Kutumia Mafuta Ya Vaseline
Urembo

Namna Nyingine Za Kutumia Mafuta Ya Vaseline 

wengi ambao tunatumia mafuta ya mgando tutakuwa tunajua mafuta haya ya Vaseline, ukiachana kuwa ni mafuta mazuri ya ngozi unaweza kutumia mafuta haya kwa mambo mengine mbalimbali na yakawa msaada mkubwa.

  • Kutoa Gundi Kwenye Frontal

Wale ambao tunabandika nywele tunajua kasheshe la kutoa gundi ya fronta,l ukiachana na kuumia lakini pia unaweza kukata au kuharibu edge’s zako,namna nzuri ya kuondokana na mateso haya ni kutumia Vaseline kutolea frontal. Paka vaseline yako kabla hujatoa frontal iache ilainishe frontal kwa muda kisha anza kubandua na utaona ni rahisi, haina maumivu na haikati edges.

  • Kutoa Big G Kwenye Nywele

Hakuna kitu king’ang’anizi kwenye nywele kama Big G, unaweza kukata nywele na kuumia ikikugandia, njia rahisi ni kutumia vaseline kupaka sehemu ambayo Big G imegandia na itatoka kirahisi.

  • Kufanya Harufu Ya Perfume Idumu

Ilikufanya perfume yako idumu muda mrefu ukiachana na kupaka perfume hio sehemu sahihi unaweza kwa kuanza kupaka Vaseline sehemu husika kisha ndio upulizie perfume na itadumu muda mrefu zaidi.

  • Inasaidia Kuondoa Magaga

Kama miguu yako imepasuka (magaga) basi unaweza kutumia Vaseline kuondoa / kupunguza tatizo hilo, safisha miguu yako vyema, kausha na kisha paka mafuta ya Vaseline ya kutosha na uvae socks, miguu yako italainika na tatizo kupungua.

Related posts