SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

NAMNA SAHIHI YA KUBADILI RANGI YA NGOZI
Skin Care

NAMNA SAHIHI YA KUBADILI RANGI YA NGOZI 

Kuna baadhi ya mada ni nyeti sana kutokana na kuwepo na mitazamo tofauti juu ya hiyo mada husika mojawapo ikiwa ni suala zima la kubadili rangi ya ngozi. Lakini hatuwezi pinga kuwa pamoja na uwepo wa mitazamo tofauti kila mtu ana uhuru wa kuamua anachokitaka juu yake na mwisho wa siku kila mtu atafanya kinachofurahisha nafsi yake. Kuliko kutogusia kabisa hili suala ni vyema kutoa mwongozo juu ya namna sahihi ya kubadili rangi kuliko kukaa kimya huku wanawake wengi wakiendelea kuharibu ngozi na viungo vya ndani kisa tu hawajui ni nini wafanye na nini wasifanye. Hili sio jambo geni, limefanywa na wengi lakini utofauti unakuja katika hatua zinazotumika ndio maana utakuta wengine wanaishia kubabuka na wengine wanapata matokeo. Tutaanzia athari za kutumia niia zisizo sahihi kisha hatua sahihi na bidhaa za kutumia.

ATHARI ZA KUTUMIA NJIA ZISIZO SAHIHI

Tuna uhakika ushawahi kukutana na mdada mweupe halafu uso mwekundu balaa. Au mdada uso umekua mweusi, uso na mwili vina rangi tofauti, au ana vipere visvyoeleweka. Basi hiyi ni intro tu, viungo vya ndani pia huathirika kutokana na matumizi mabovu ya dawa na vipodozi kwa ajili ya kubadili rangi ya ngozi. Kuna kuharibika kwa maini na figo. Kuna unene unaotokana na vipodozi hususani vyenye steroids, mara nyingi mtu hunenepa maeneo ya tumbo na kiuno zaidi. Pia kuna kupata michirizi ambayo ni migumu sana kutoka. Ubaya wa vipodozi hivi ni kwamba vinatoa matokeo ya haraka na wakati mwingine matokeo huwa mazuri sana kwa muda lakini baadae mtu huja kuharibika. Hizo ni baadhi ya athari. Kuna hatua tano za muhimu katika kubadili rangi. Nakuomba ujifunze zaidi kupitia mitandao na watu wengine maana ni ngumu kugusia kila mada kwa undani zaidi lakini nitajitahidi kuelezea kadri niwezavyo. Hatua hizo ni zifuatazo;

KUJITATHMINI

Najua labda hukutegemea hili,ila ni muhimu kujitathmini. Una rangi gani na unataka kufikia rangi gani? Unafanya hivi kwa ajili ya nani? Je ni mpenzi? Au unataka kushindana na mtu ulomuona? Kama ni hivyo basi nakuomba usibadili kitu. Usifanye kitu kisa mtu mwingine, hakikisha umeridhia na unataka kujibadili kwa sababu unapenda mwenyewe na unaona utapendeza zaidi ukiwa na shade flani na sio vingine.

EXFOLIATION (Kuondoa ngozi iliyokufa)

Kuna bidhaa nyingi ukitumia huoni matokeo, wakati mwingine hii inatokana na ngozi iliyokufa. Unapoondoa ngozi iliyokufa basi unasaidia unachopaka kupenyeza kwenye ngozi na hivyo kukupa matokeo. Pia inasaidia bidhaa kufanya kazi kwenye kila eneo ili upate rangi inayowiana mwili mzima. Unatakiwa kufanya exfoliation kwa wiki sita. Exfoliation ndio itakayokupa rangi moja.

Exfoliation hufaywa kwa njia ya kemikali na njia ya kujisugua. Kwenye kujisugua hapa unajisugua mwili mzima kwa scrub, usisugue uso kila siku mara mbili au tatu kwa wiki inatosha. Mwili unaweza usugua zaidi. Kwa kemikali kuna lotion zinatengenezwa kwa ajili ya kuondoa ngozi ilokufa. Utakuta imeandikwa with AHA au with AHA and BHA. AHA na BHA ni acid flani ambazo husaidia kuondoa ngozi ilokufa. Mfano wa hizi acid ni lactic acid na fruit acid. Mfano wa hizi lotion ni Amlactin, Fair and white Aha,palmers smmothing lotion n.k.Kuna namna ya kujitengenezea mweyewe pia. Ni rahisi kununua mtandaoni, ili upate dukani inabidi uangalie ingredients za lotion moja baada ya nyingine au utafute exfoliating lotion. Cheki youtube namna ya kutengeneza lactic acid lotion. Mwishoni ntaweka website za kujifunza zaidi kuhusu masuala haya.

BIDHAA SAHIHI

Bidhaa sahihi ni lotion zote au tube au serum zisizo na steroids. Utakuta kwenye package au kopo kuna vitu kama betamethasome na clobetasol propionate,jua hizi ni steroids. Hizi ni baadhi tu, lakini zote huwa na maelezo kuwa ni dawa na isitumike zaidi ya muda flani kwenye karatasi ya ndani. Usitumie lotion ambazo umeona zina madhara kwa wengine, kuna lotion zinajulikana kuharibu watu kama carolight. Ukinunua bidhaa ukaona dalili mbaya acha kuitumia mara moja. Tumia bidhaa zenye vitu asili kama vitamin c, kojic acid, goat milk, fruit acids, mulberry extract, glutathione, sepiwhite, licorice, papaya extract, hydroquionone kwa kiwango kidogo na vinginevyo.

KUJIKINGA NA JUA (Sunscreen and sunblocks)

Watu wenye ngozi nyeupe hususani wazungu hutumia sunscreen au sunblock. Bila ulinzi ngozi yao uungua kwenye jua au uwa inakuwa nyekundu. Nadhani ulishawahi kusikia neno sunburn, mtu anapounguzwa na jua anapata sunburns. Wale wadada unaowaona wana sura nyekundu au wamechomwa muda mrefu mpaka wamepata makovu meusi usoni wana sunburns. Kemikali nyingi haramu kwa kubadili rangi hufanya ngozi kuwa laini na nyepesi sana. Kwakuwa kubadili rangi kuwa mweupe ni kupunguza melanin pigments ambazo hulinda ngozi isiunguzwe na jua basi inakuwa rahisi kwa ngozi kuungua inapopigwa na jua. Unaweza usione madhara ya jua hapo kwa papo lakini jua kiasi tu linaweza sababisha upate makovu ikiwa unatumia bidhaa zisizofaa.Basi kama unabadili rangi hakikisha unanunua sunscreen au sunblock.

Pia jua husababisha chembechembe za melanin ziongezeke, chembechembe hizi ndio hufanya ngozi ionekane nyeuse hivyo kuondoa matokeo. Sunblock ni nzuri zaidi maana inakinga miale aina zote. Sunscreen na sunblock hutofautiana uwezo, zinaanzia spf 15 na kuendelea. Tumia sunscreen yenye spf zaidi ya 40.Kiwango cha Spf huwa kimeandikwa kwenye kopo la sunscreen. Paka sehemu zote za mwili.

KUJENGA NGOZI (Skin building)

Kwakuwa bidhaa nyingi za ngozi hupunguza uzito wa ngozi hata bidhaa sahihi. Pia exfoliation hupunguza uzito wa ngozi basi ni muhimu kupaka mafuta yanayoipa ngozi rutuba kama mafuta ya nazi, shea butter, cocoa butter au skin building lotion (lotion zenye virutubisho na vitamin zinazojenga ngozi). Hii itasaidia uwe na ngozi yenye afya na inayong’aa na kuvutia. Unatakiwa pia utoe siku za kupumzisha ngozi. Mwanzoni unaweza kupumzika siku moja. Kwenye hii siku haupaki bidhaa za kubadili ngozi bali unapaka bidhaa za kujenga ngozi tu.

KUTUNZA MATOKEO (maintaining results)

Unapoanza Kutumia bidhaa unafanya exfoliation kwa wiki sita. Kisha unaanza kutumia lotion, mafuta au serum za kubadili rangi siku sita kwa wiki huku ukipumzika siku moja. Unajenga ngozi siku tatu au zaidi. Yani baada ya kupaka lotion na kuiacha kwa dakika tano unapaka skin builder. Baada ya wiki sita za mwanzo siku zinazofuata unafanya exfoliation mara tatu kwa wiki.

Imeandikwa na @Raymimie

 

Unaweza jifunza zaidi kupitia website hizi

https://www.realself.com/Skin-lightening/info

http://www.skinalley.com/forums/skin-lightening.5/

http://www.skincaretalk.com/forum.php#/forums/12

Related posts

5 Comments

 1. ดูดวงยูเรเนียน

  … [Trackback]

  […] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-sahihi-ya-kubadili-rangi-ya-ngozi/ […]

 2. 무료 다시보기

  … [Trackback]

  […] Here you will find 14915 additional Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-sahihi-ya-kubadili-rangi-ya-ngozi/ […]

 3. one up shroom chocolate​

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-sahihi-ya-kubadili-rangi-ya-ngozi/ […]

 4. best dark chocolate raspberry​

  … [Trackback]

  […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-sahihi-ya-kubadili-rangi-ya-ngozi/ […]

 5. หวยออนไลน์

  … [Trackback]

  […] Here you can find 45535 more Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-sahihi-ya-kubadili-rangi-ya-ngozi/ […]

Comments are closed.