SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kukabiliana Na Midomo Mikavu
Urembo

Namna Ya Kukabiliana Na Midomo Mikavu 

Moja ya changamoto kubwa unayopitia Wakati huu wa baridi ni kuwa na lips kuvu na wengine kukatika na kufanya Vidonda Kabisa. Kama sio wewe ni jirani yako. Remedies zifuatazo inaweza kuwa suluhisho la tatizo lako. 


Kabla ya kuendelea na “home remedies” ni muhimu uelewa kuwa Kama unahitaji Ubora wa Urembo wako Unatakiwa kunywa maji ya kutosha. Home remedies na vipodozi vyote utashindwa kupata matokeo bora kwa sababu ya kiwango kidogo cha maji unachokunywa. Hivyo basi kunywa maji angalau bilauri 8 kwa siku. Pia ni muhimu  ufahamu sababu za ukavu wa lips

 • Kuramba midomo yako kwa kutumia Ulimi. Mate yana uwezo mkubwa wa kukausha midomo yako 
 • Kuathiriwa na mwanga wa jua 
 • Kuvuta sigara na kunywa pombe 
 • Vichubua ngozi vinavyopatikana mfano kwenye Dawa za meno 
 • Uzio ” allergies”
 • Baadhi ya madawa. 

Baada ya kuona sababu zifuatazo ni home remedies uweze kujisaidia. 


1. Cocoa Butter 

Hapa unaweza kutumia cocoa butter, Shea butter, Peanut Butter, yoghurt, butter milk. Chukua Cocoa butter au Shea butter weka kwenye lips zako, lala nayo. Fanya hivyo kila siku hadi uone matokeo. Ukiamua kutumia Peanut butter, yoghurt, na butter milk unaweka kwenye lips kwa dakika 15 Kisha osha kwa maji ya kawaida. (utachafua Shuka zako, Usilale nayo) 
2. Alovera Alovera

ina virutubisho muhimu vinavyohitajika Kwa Ngozi yako. Utahitaji jani moja la alovera. Chukua alovera Kata jani lake vipande vipande toa gel yake Paka kwenye lips. Unaweza kulala nayo. Tumia hadi uone matokeo. 
Tahadhari : alovera ni chungu, kuwa muangalifu Unapotumia. 


3. Mafuta ya Asili. Mafuta ya asili Kama vile 

 • Mafuta ya Nazi 
 • Jojoba oil 
 • Mafuta ya zaituni 
 • Mafuta ya parachichi 
 • Mafuta ya mnyonyo ( castor oil) 
 • Mafuta ya Tangawizi 
 • Mafuta ya Lozi (almond) 

Mafuta yote hayo yana uwezo wa kukuondolea ukavu wa lips. Chukua aina moja ya mafuta, weka kwenye lips zako. Rudia hadi uone matokeo. 


4. Mafuta ya Nazi na Sukari

Sukari kijiko kimoja Mafuta ya Nazi vijiko 3.Changanya kupata mchanganyiko, weka kwenye lips. Acha baada ya dakika 20 Osha na maji ya kawaida. Rudia hadi uone matokeo. 
5. Majani ya waridi “rose” na maziwa fresh

 Chukua majani ya waridi kiasi Changanya na maziwa saga kupata mchanganyiko mzito. Weka kwenye lips mchanganyiko huo kwa dakika 20. Osha na maji ya kawaida. Rudia hadi uone matokeo. 


6. Tango 

Tango lina virutubisho vya kutosha. Unachotakiwa kufanya ni Chukua tango moja Kata vipande vidogo vidogo kwa mduara weka kwenye lips zako. Baada ya dakika 30 osha. 


7. Pia Unaweza kutumia Lip balm kutoka kwa Duka au Muuzaji unaemuamini. 


8. Tumia lipstick zenye SPF kuanzia 15 hadi 30 kulinda lips zako zisipatwe na mwanga wa jua na kuwa kavu. SPF (sun protecting factor) kilinda jua. 


9. Acha Kuramba ramba lips zako na Ulimi, mate yanasababisha ukavu zaidi kwenye lips. Ongeza bidii ya kunywa maji zaidi. 


Jee wewe utafanya ipi Kati ya hizo!?  Shea na uwapendao!
©binturembo

Related posts