SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kuondoa Madoa Meusi Usoni Bila Kutumia Vipodozi Vikali
Skin Care

Namna Ya Kuondoa Madoa Meusi Usoni Bila Kutumia Vipodozi Vikali 

Kwanza kabisa naanza na  kesi ya madoadoa mwilini. Iwe ya usoni yaliyotokana na chunusi au Sehemu zingine za mwili kutokana na upele, vidonda na kadhalika.

Katika mazingira kama hayo ushauri ufuatao utakufaa:

  • Kadiri muda unavyoenda ngozi yako Itakuwa inajitengeneza vizuri yenyewe na hivyo madoadoa hayo yatakuwa yanafifia Pole Pole na hata hatimaye kupotea kabisa kutegemea na umri wako, lishe yako, ulipata ukiwa na umri gani na ni madoadoa au makovu ya ukubwa gani.

Ukiwa na umri mdogo mwili hukua na kufanya ukarabati haraka haraka hivyo madoadoa huwai kupungua na kuisha; ukiwa unakula vizuri nyama, mayai, maziwa, maini, samaki, kuku, maharage na vyakula vingine vya protini unapata protini ya kutosha na madoadoa yanawahi kuisha; madoadoa madogomadogo yanawahi kufifia na kuisha; kwa hiyo unaweza kula vizuri na kuwa mvumilivu tu na madoadoa yako yakapungua na kuisha…..

  • Unaweza kuharakisha madoadoa kuisha kwa kutumia vipodozi ambazo husaidia ngozi kujitengeneza upya na kuondoa ngozi ya zamani yenye madoadoa. Bio oil ni miongoni mwa dawa na vipodozi ambavyo husaidia kupunguza na kuondoa madoadoa na makovu. Unachotakiwa kufanya ni kuwa makini sana na utumiaji na kununua kutoka kwa wauzaji wanaoaminika

Faida Na Matumizi Ya Mafuta Ya Bio-Oil

  • Kupaka make-up na makorokoro mengine ili kuficha madoadoa ni kupoteza pesa nyingi maana haiondoa madoadoa na bado gharama yake ni kubwa kiasi cha kutosha kuondoa kabisa madoadoa yako

Kwa kusema ukweli kila tatizo la ngozi, lina vipodozi vya kulimaliza; isipokuwa tu watu wanakosa matokeo mazuri kwa sababu ya kufuata ushauri mbaya na kutotumia vipodozi maalum kwa ajili ya tatizo husika na ngozi husika

Kwa hiyo kama unasumbuliwa na madoadoa Leo nakupa nguvu na uhakika kwamba unaweza kumaliza madoadoa yako yote, kupendeza na kung’aa kama zamani 

Usitumie vipodozi vikali, hakuna haja ya kuharibu ngozi yako nzuri kwa fedha yako  mwenyewe wala kujificha kwa Hijabu, Suruali na Make Up
Pata ushauri mzuri, kuwa chini ya muangalizi mwenye uelewa mzuri wa  vipodozi na tumia bidhaa nzuri. Kingine Uwe mvumulivu!
Baada ya hapo utapata matokeo yoyote mazuri unayoyataka. 

@binturembo

Related posts