SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kuondoa Madoa Meusi Usoni
Skin Care

Namna Ya Kuondoa Madoa Meusi Usoni 

Madoa meusi (black spots) usoni ni jambo ambalo linawasumbua wanawake wengi sana na hupelekea mtu kutokujiamini na mara nyingine kujidharau, kujichukia na kukosa ujasiri wa kuwa bila ya make up “off make up”. Hili tatizo husabaishwa na vitu tofauti,hivyo kujua chanzo cha tatizo ni muhimu sana.

Sababu zinazosababisha madoa meusi usoni ni kama ifuatavyo;


1.Hyperpigmentation

Hili tatizo linatokea pale ngozi inapoharibiwa katika eneo fulani,hivyo husababisha ngozi kutengeneza ‘melanin’ nyingi na kusababisha eneo hilo kuonekana nyeusi kuliko nyingine.


2.Homoni kutokuwa katika kiwango sahihi katika mwili(Hormonal imbalances)

Pia hili husababisha madoa meusi usoni, na hili linaweza tokea wakati wa ujauzito,kwa watu wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango(control pills) na pia mwanamke anapoingia katika kipindi cha ukomo wa kuzaa(menopause).


3.Kukaa juani kwa muda mrefu(excessive sun exposure).

Pia hii hutokea kwasababu mwili unaanza kutengeneza ‘melanin’ kwa wingi ili kuzuia kuharibiwa kwa ngozi na mionzi ya jua. Na hapo Ndio utaona madoa meusi usoni 


4.Chunusi

Pia hutokea kwa watu ambao wana tatizo la chunusi. Wengi wenye chunusi huwa na tabia ya kutumbua chunusi na Kwa kufanya hivyo chunusi hupona kwa kubakiza kovu jeusi usoni. Mara nyingi haya madoa meusi yanapotea baada ya muda fulani kupita,lakini muda mwingine inaweza ikawa ni ngumu kupotea yenyewe kutokana na aina hizo za chunusi. Na Hapo Ndio Mwanamke huanza kujichukia na kujiona Hafai.


Kama Umekuwa na tatizo hili kwa muda mrefu, usijali Leo hapa hapa utajua nini cha kufanya ukiwa nyumbani kwako. 


Jinsi ya kuondoa madoa meusi ukiwa nyumbani

 • Tumia juice ya aloe vera

paka sehemu yenye madoa meusi mara mbili kwa siku. Fanya hivi kwa wiki kadhaa na utashuhudia mabadiriko makubwa.

 • Asali na sukari

Changanya asali na sukari hii ya kawaida na ujifanyie ‘massage’ mara mbili kwa wiki. Hii husaidia kuondoa chembechembe za ngozi zilizokufa na kufanya ngozi mpya na hivyo kuondoa madoa meusi.

Njia Asili Ya Kuondoa Madoa Yaliyo Tokana Na Chunusi

 • Tumia matunda ambayo yana uwingi wa vitamin C na E

Matunda kama machungwa yana vtamin C ambavyo ni Antioxydant na pia hupunguza melanin isitengenezwe kwa wingi na hivyo kufanya ngozi isiwe na madoa meusi. Pia matunda ambayo yana vitamin E kwa wingi ni muhimu kuyatumia ,mfano Carrots.

 • Tumia sunscreen cream

.Hizi cream huzuia mionzi ya jua ambayo ni chanzo mojawapo cha madoa meusi usoni, kwa hiyo hakikisha unatumia sunscreen cream kabla ya kutoka kwa ajili ya matembezi ya hapa na pale.
Hizo ni “home remedies” huleta matokeo mazuri sana, ila bahati mbaya hayaji kwa muda mfupi. Unatakiwa kuwa Mwaminifu na mvumilivu! 

Umuhimu Wa Kupaka Sunscreen Katika Ngozi


Pia ukiona madoa yako hayatoki unaweza ukamwona mtaalam wa ngozi kwa ajili ya ushauri na matibabu zaidi.
Jee ni nini utafanya Kati ya hayo tuliyoeleza Hapo juu!? Tuambie kwenye Comment hapo chini. 

@Binturembo

Related posts

5 Comments

 1. Plantation Shutters

  … [Trackback]

  […] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-madoa-meusi-usoni/ […]

 2. download video tiktok

  … [Trackback]

  […] Read More on that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-madoa-meusi-usoni/ […]

 3. Best Psychedelic Store Perth

  … [Trackback]

  […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-madoa-meusi-usoni/ […]

 4. 대구웨딩홀

  … [Trackback]

  […] Find More here on that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-madoa-meusi-usoni/ […]

 5. Dr Stacy Pineles and David T Bolno

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-madoa-meusi-usoni/ […]

Comments are closed.