SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kuondoa Weusi Mwilini Kwa Kutumia Scrub Ya Kahawa
Skin Care

Namna Ya Kuondoa Weusi Mwilini Kwa Kutumia Scrub Ya Kahawa 

Watu wengi wana uchafu kwenye ngozi hata wakioga bila kujua sababu ni nini, wengine wanakuwa na weusi flani hata kama ni mweupe. Utasikia mtu anasema flani haogi vizuri, siyo kweli ni ngozi inakuwa imechoka.
Scrub nzuri ya kuondoa weusi huo ni sukari na  mafuta ya mzaituni ambayo inapakwa kisha unafanyia masaji mwili mzima kuondoa uchafu wa ngozi.


Jinsi ya kuandaa

 • Chukua kahawa vijiko viwili vikubwa,
 • kijiko 1 kikubwa cha sukari
 • mafuta ya mzaituni vijiko vinne.

Changanya vyote kwa pamoja upate mchanganyiko. Baada ya hapo, chukua mchanganyiko huo paka mwilini mwako, ufanyie mwili masaji kama unayesugua sehemu hasa sehemu nyeusi, zoezi hilo lifanye wakati unaoga.
Nikisema sehemu nyeusi namaanisha kwenye maungio, makwapani na shingoni, hizi ni sehemu ambazo weusi wake huwa unazidi hivyo kwa kutumia mchanganyiko huu unaweza kurudisha rangi asili ya ngozi yako.
Kwa wanaotaka kung’arisha miguu scrub hii pia ni nzuri, inafaa kwa asilimia kubwa. Scrub hii inafaa kwa sehemu yote ya mwili isipokuwa usoni tu.


Vile vile Kahawa ina matumizi mengine Kama kuondoa michirizi na chunusi Kama ifuatavyo :


Scrub ya Kahawa kwa michirizi.


Chukua Kahawa na mafuta ya Nazi , changanya vizuri kisha itumie kama scrub nyingine katika sehemu ambapo una michirizi.
Scrub pole pole kwa kuzunguka “circular motion” kwa Muda wa dakika 10-15. Kisha nawa kwa maji ya uvuguvugu. Kausha Kisha paka moisturizer.


Scrub ya kawaha kuondoa Chunusi.


Vitu unavyohitaji ni Kahawa Mafuta ya Nazi Na Mdalasini.
Changanya vizuri kiasi sawa kwa Kila kitu.
Paka usoni na uwe kama unasugua polepole kwa Muda wa dakika 5-10.
Nawa uso kwa maji ya uvuguvugu Kisha paka moisturizer.
Fanya mara 2 kwa wiki  kwa miezi 3. Utaona matokeo mazuri.
Wanatumia wenye ngozi Aina Zote na umri wowote!
Jee umewahi kutumia Kahawa Katika urembo, unatumiaje?
Shea na uwapendao 
©binturembo 

Unaweza kupata mafuta ya nazi bora kutoka kwetu @afroswaggaoils au tupigie kupitia 0765 768 667

Related posts

4 Comments

 1. สล็อตวอเลท ไม่มีขั้นต่ำ

  … [Trackback]

  […] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-weusi-mwilini-kwa-kutumia-scrub-ya-kahawa/ […]

 2. Investment

  … [Trackback]

  […] Read More here on that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-weusi-mwilini-kwa-kutumia-scrub-ya-kahawa/ […]

 3. Asbestos Abatement Hertel

  … [Trackback]

  […] Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-weusi-mwilini-kwa-kutumia-scrub-ya-kahawa/ […]

 4. 다시보기

  … [Trackback]

  […] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-weusi-mwilini-kwa-kutumia-scrub-ya-kahawa/ […]

Comments are closed.