SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kuondoa Weusi Wa Macho “Miwani /Puffy Eyes )
Urembo

Namna Ya Kuondoa Weusi Wa Macho “Miwani /Puffy Eyes ) 

Weusi chini ya macho unasababishwa na mambo mengi ikiwamo kukosa usingizi wa kutosha. Binadamu anatakiwa kulala masaa yasiyopungua 6 hadi 8, kuhakikisha ubora wa afya na Ngozi yake. 
KULALA na kupumzika ni muhimu kwa kuwa na afya nzuri na muonekano mzuri. Hata hivyo, aghalabu huwa sio rahisi kuupata usingizi wa kutosha kila usiku na wakati mwingine utaona weusi usoni chini ya macho unapokosa usingizi. Hali hii pia husababisha ‘puffy eyes’ yaani uvimbe wa aina fulani katika sehemu karibu na macho.

  • Viazi


Viazi vina asili ya enzymes zinaong’arisha ngozi, ambao husaidia kufifiza weusi chini ya macho.Weka kiazi kibichi katika hiyo sehemu ya machoni unaweza kukikata vipande vidogo vyembamba au kwa kusaga kupakaa rojo.Weka kwa 30 dakika kisha toa,osha uso kwa maji ya kawaida.

  • Majani ya Nanaa “Mint” 


Yaponde majani ya mint kidogo na pakaa chini  macho hapo kwa dakika tano. Safisha uso kwa maji ya kawaida. Unaweza ukatumia majani ya mint ukachanganya na asali au olive oil kabla hujapakaa kwenye macho. Baada ya kuosha, paka ‘moisturizer’.

  • Tea bags


Caffeine ilioko ndani ya  majani ya chai ina uwezo wa kukazisha ngozi chini ya macho na pia huondoa kuungua na mbadiliko wa rangi. Baada ya kutumia tea bag yako  weka kwenye friji ipate baridi. Kisha Chukua tea bags zako mbili kutoka kwa friji weka kwenye macho yako yakiwa yamefungwa kwa kuilaza kwa dakika 15.

  • Rose water


Rose water ina vitamini kama A na C, Unapaswa kuyapaka hayo maji chini ya macho kwa dakika 10 kwa kutumia pamba.

  • Matango


Kuweka vipande vya  matango ya baridi kwenye kila jicho husaidia kuondoa uchovu, na husaidia kulainisha ngozi ya machoni. Matango pia hufanya kazi ya kukaza na kung’arisha uso, husaidia kuondoa mabadiliko ya rangi katika ngozi.

Ni vizuri zaidi kutumia Njia moja kwa muda ili uweze kujua ni ipi hasa inakufaa! Rudia hadi uone matokeo unayotaka! 
Jee wewe Utachagua ipi, Kati ya hizo Hapo juu!?  Tuambie zaidi kwenye comment hapo chini.

Imeandikwa na @binturembo 

Related posts

4 Comments

  1. browse around this site

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-weusi-wa-macho-miwani-puffy-eyes/ […]

  2. weed delivery brampton

    … [Trackback]

    […] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-weusi-wa-macho-miwani-puffy-eyes/ […]

  3. เว็บคาสิโนออนไลน์

    … [Trackback]

    […] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-weusi-wa-macho-miwani-puffy-eyes/ […]

  4. magic mushrooms dried for sale​

    … [Trackback]

    […] Here you will find 63630 more Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kuondoa-weusi-wa-macho-miwani-puffy-eyes/ […]

Comments are closed.