SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kupata Mikono Laini
Urembo

Namna Ya Kupata Mikono Laini 

Kazi nyingi tunafanya kwa kutumia mikono, kupika, kufua, kuosha vyombo n.k kazi hizi husababisha mikono yetu kuwa migumu, kuna ambao wanajisikia vibaya kuwa na mikono migumu wakisahau kuwa ni kazi muhimu ndizo ambazo zimesababisha iwe migumu, sio jambo la ajabu kuwa na mikono migumu it shows unafanya kazi. Lakini unaweza kurudisha mikono yako kuwa laini kwa kufanya haya.

  • Osha mikono yako kwa moisturizing soap

Kuna sababuni ukitumia zinafanya mikono kuwa mikavu zaidi, achana nazo tumia sabuni ambazo zitakusafisha mikono lakini pia hazifanyi mikono yako kuwa mikavu bali zinakupa unyevu na kukuacha na unyevu.

  • Paka Lotion / Mafuta Kilasiku

Unaweza kuwa unapaka mafuta mwilini na ukahisi yale unayoyapaka mwilini yanatosha yaani kwasababu umetumia viganja kupaka mafuta basi yaleyale yaliyobaki kidogo kiganjani ukadhani yanatosha, hakikisha unapaka mafuta ya kutosha viganjani kwako pia.

  • Beba mafuta / hand lotion

Ikiwa tunafanya kazi mbalimbali pia utaingia maliwatoni utanawa mikono, utakula utanawa mikono na kuiacha mikavu hakikisha unabeba mafuta au hand lotion na kila unapo jisafisha mikono yako unapaka.

  • Paka Suncreen Cream

Mikono inakuwa exposed na jua pia inaweza kuharibu ngozi yako ya mikono, hakikisha unapaka SPF mikononi pia.

Related posts