SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kupendezesha Vidole Vyako Vya Miguu
Urembo

Namna Ya Kupendezesha Vidole Vyako Vya Miguu 

Kuna vitu ambavyo kila mmoja wetu ana insecurity navyo katika miili yetu, wengine inaweza kuwa mikono, tumbo, shingo, macho nk ili mradi tu kuna kitu ambacho una notice hakipo sawa. Wachache wanachukua muda wao kutafuta namna ya kutafuta solution ya majibu haya wakati wengine tunaamua kuvificha visionekane.

Tulisha wahi kuongelea hili swala unaweza kubonyeza hapa kusoma namna ambavyo unaweza ku-handle insecurity zako mwili katika upande wa fashion.

Leo tunaongelea kuhusu kucha au vidole vya miguu ambapo mates wetu wengi wanalalamika kwamba hawawezi kuvaa viatu vya aina fulani sababu ya vidole vyao kukosa mvuto,mfano vidole vifupi, kucha mbaya nakadhalika. Leo tunawaletea namna ya kudeal navyo

  • Jifunze kuvipenda

Hii ni step muhimu sana, kama hutojifunza kuvipenda vidole vyako namna vilivyo huwezi kuvifanya vikawa na mvuto, mara zote ukiviona utataka uvifiche tu kwa sababu huvipendi utavipuuza na kuvificha kwenye raba au viatu vya kufunga na hii itapelekea kutokuvisafisha na kuvifanya vizidi kuonekana vibaya. Kwaio hatua ya kwanza ni kuvipenda kumbuka wewe unacho kuna mwingine hana na anatamani angekuwa nacho hata hiko ambacho wewe unakiona kibaya.

Penda kucha zako

  • Vifanyie Usafi

Kila kitu kinakuwa less unattractive kikifanyiwa usafi, hakikisha unasafisha vidole vyako hata mara mbili kwa week, iwe kwa kwenda salon kufanyiwa usafi au kwa kujifanyia mwenyewe nyumbani. Kama si mpenzi wa kucha ndefu kata kucha lakini hakikisha ni safi na usifanye zisionekane kabisa.

Ng’arisha kucha kwa kutumia vitu vya asili

  • Paka rangi au henna

Kama ni mpenzi wa rangi au henna basi kuwa unapaka mara kwa mara ili kuvipa mvuto zaidi, rangi ni kama makeup ya kucha, vile ambavyo una paka makeup kufanya uso wako uvutie zaidi basi ni sawa sawa na rangi ya kucha au henna, ilikuvipa vidole vyako vya miguu mvuto hii ni njia nzuri zaidi.

  • Accessories

Sasa hivi kuna accessories za miguu kama pete za miguu au hata vikuku, vikuku havivaliwi vidoleni lakini ni namna ambavyo vinakaa na kuvutia vinaweza ku-highlight mguu wako na kufanya eneo hili zima kuonekana na mvuto. Lakini pia pete za vidole vya miguu nazo huvipa vidole muonekano mzuri.

Well afromates tuambie huwa unatumia njia ipi kupendezesha vidole vyako vya miguu?

Related posts

3 Comments

  1. over at this website

    … [Trackback]

    […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kupendezesha-vidole-vyako-vya-miguu/ […]

  2. Dark web market links

    … [Trackback]

    […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kupendezesha-vidole-vyako-vya-miguu/ […]

  3. 코인선물

    … [Trackback]

    […] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kupendezesha-vidole-vyako-vya-miguu/ […]

Comments are closed.