kunazile siku ambazo tunaona tunahitaji kupumzisha kichwa na ma-wig na weaving’s na kuamua kusuka tu simple hair style, kwasasa wengi wetu huwa tunachagua hii minyoosho hair style yenye rasta, ni simple na elegant unaweza kuvalia chochote iwe suit, casual etc.
Lakini haimaanishi basi ukisuka nywele hizi uzitegemee tu zenyewe unahitaji kufanya vitu vichache ili kunyanyua muonekano wako
Makeup / Weka Ngozi Vizuri
Ikiwa style ya nywele ni simple ni vyema ukahakikisha uso wako unakaa vyema ili kunyanyua muonekano wako, paka makeup hata simple ila kama sio mpenzi wa makeup basi hakikisha umepaka mafuta vyema una lipstick au lip balm

Style
Yes unaweza ku-style minyoosho yako kama umesuka na rasta unaweza ukaachia mikia, ukabana, unaweza kuleta mikia upande mmoja mbele lakini pia zipake mafuta vyema na weka edges vizuri mbele kwa kupaka gel na kuzi-style vizuri.
Accessories
Unaweza kuvaa hereni, mkufu, au miwani hii itanyanyua muonekano wako ki-ujumla na kupata muonekano mzuri, nywele zikiwa simple na huku huna accessories unaweza kuonekana basic zaidi, makesure umevaa kimoja au viliwi kati ya tulivyo vitaja.

Vaa Vizuri.
Unamtoko na umesuka twende kilioni usi-cancel kwenda kuwa creative katika mavazi yako upendeze, watu watasahau kuhusu nywele na ku-concentrate on mavazi yako
Well ni matumaini yetu uta slay minyoosho yako kuanzia sasa.
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…