SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kutambulisha Kipodozi Kipya Cha Ngozi Katika Ngozi Yako
Urembo

Namna Ya Kutambulisha Kipodozi Kipya Cha Ngozi Katika Ngozi Yako 

Inawezekana una skincare routine lakini unataka kuongezea kipodozi kingine au pia inawezekana ni mara ya kwanza kuwa na skincare routine je unaanzaje kutambulisha kipodozi hiko kipya katika ngozi yako?

Katika kila kipodozi kuna ingredients ambazo zinaweza ku-react vyema au vibaya katika ngozi yako inabidi uwe muangalifu pale unapo taka kuanza kutumia kitu kipya unachotakiwa kufanya ni,

  • Chagua kipodozi kutokana na aina ya ngozi yako

Usianze tu kutumia kipodozi kwasababu fulani anakitumia na kina mpenda, hakikisha unajua skin type yako na kipodozi kipi kinaendana na ngozi yako.

Normal Skin – ni ile ngozi ambayo ipo well balanced na yenye afya, una small pores na hupati matatizo ya ngozi mara kwa mara.

Dry skin – ni aina ya ngozi ambayo mara nyingi unasikia ni tight na parche hii mara nyingi hutokewa na fine lines na flakiness

Oily Skin – aina hii ya ngozi ni ile yenye mafuta mengi na una pata matatizo ya ngozi mara kwa mara

Combination skin – hii ni ile una ngozi kavu maeneo mengine lakini kwenye pua, kidovu na paji la uso kuna mafuta.

  • Jua Kuhusu Athari Za Viungo Vilivyopo Katika Kipodozi

Ikiwa kwasasa kuna vipodozi vingi vya ngozi ni rahisi kushawishika na kununua kila kitu unacho kiona, kabla ya kuvitumia jua kwamba kuna baadhi ya bidhaa na viungo vilivyopo kwenye bidhaa hizo vinafanya kazi vyema kwa pamoja na kuna ambavyo hutakiwi kuvichanganya, kabla ya kuvipaka kwenye ngozi yako jifunze kipi kina enda na kipi na kipi hakiendani ili kuepusha kuharibu ngozi yako.

Note huitaji kukesha kujua kila aina ya kiungo kilichopo kwenye kipodozi chako ila angalia zile main ambazo zipo kwa asilimia kubwa kwenye kipodozi hiko.

  • Anza Kwa Kufanya Majaribio Kabla Ya Kupaka Usoni

Hii inaitwa skin patch test, anza kwa kupaka kipodozi chako sehemu ambazo hazionekani mara nyingi ina shauriwa upake ndani ya mkono yaani maeneo ya karibu na kwapa kwa ndani sio nje. Paka hiko kipodozi sehemu hio na kiache kwa masaa 24 bila ya kukifuta, ukiona hakuna tatizo unaweza kujaribu tena sehemu nyingine kama chini ya taya kiache kwa kwa muda then unaweza kupaka usoni lakini hii pia haimaanishi hiko kipodozi hakito kuharibu ila kinga bora kuliko kuanza kabisa bila ya kufanya testing

  • Muda

Anza na kipodozi kimoja kabla ya kingine, sio unanunua skin care products na unazianza zote kwa pamoja mwishoe hujui kipi kimekuharibu na kipi kimekupenda, usikurupuke anza na kimoja kipe muda hata week ndio uongeze na kingine.

Hii ni muhimu kwasababu

Ukipata breakout unajua ni kipi kimesababisha, na uanze kufanyia kazi kipi.

Kuanza product mpya kwa wakati mmoja kunaweza ku-shock ngozi yako na kuleta madhara & hatutaki hilo litokee.

  • Anza Na Product Sample

Kabla hujanunua kopo kubwa la kipodozi hiko kwa bei ghali anza na kopo dogo na angalia matokeo yake ndipo ununue kikubwa ili kuepusha hasara endapo hakito fanya kazi.

Well all in all anza taratibu na uipe muda ngozi yako ku adjust na kuzoea vipodozi vipya. tumia kipodozi mara moja au mbili kwa week halafu uanze kukitumia mara kwa mara, sote tunataka majibu ya haraka lakini kuanza kila kitu kwa mara moja kunasababisha madhara zaidi kuliko kuleta matokeo mazuri, jipe muda.

Related posts