SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kutumia Baking Soda Kupata Clear Skin
Skin Care

Namna Ya Kutumia Baking Soda Kupata Clear Skin 

Kila mtu anapenda kupata ngozi nzuri, ile ngozi inayo glow na kuvutia wengi tunatumia bidhaa za ngozi mbalimbali zenye kuleta madhara mbeleni lakini kumbe tunavitu katika majiko yetu ambayo yanaweza kutusaidia tena bila kuleta madhara makubwa.

Baking soda ni moja ya vitu ambavyo ni marachache kukosekana katika nyumba za watu mbalimbali, ina matumizi yake jikoni lakini pia inasaidia sana katika mambo ya urembo, iwe nywele, ngozi au meno leo tunakuletea namna unavyo weza kupata clear skin kwa kutumia baking soda.

 

Mahitaji: 

  • baking soda – nusu kikombe
  • maji – kikombe kimoja
  • mafuta ya nazi – kijiko kimoja cha chai
  • bakuli dogo
  • kijiko

 

Namna ya kufanya: 

Weka baking soda yako katika bakuli, mimina mafuta ya nazi na maji na uchanganye ili upate uji/paste hakikisha haiwi laini sana ili kuweza kukaa vizuri katika ngozi, paka katika sehemu ambayo ungependa iwe na clear skin na u-scrub taratibu ukisha ridhika osha kwa maji ya baridi na upake mafuta yako ya kila siku, fanya hivi mara mbili kwa week kwa matokeo mazuri.

 

Note: Usi – scub sana katika ngozi unaweza kujichubua na pia husiiache ikaukie katika ngozi.

Related posts