Kila mwanamke katika maisha yake huwa kwa namna moja au nyingine anafikiria kuolewa. Kuolewa ni moja ya ibada iliyodhihirishwa katika vitabu vitukufu vya dini tofauti. Na kila mwanamke anafurahi wakati anasubiri jambo hilo kwa hamu. Kama wewe ni bi harusi mtarajiwa na unataka utokee vizuri siku yako hiyo kubwa hizi hapa dondoo na videkezo 12 vya utunzaji wa ngozi yako pamoja na urembo ili upate kumbukumbu nzuri utakayoikumbuka siku zote za maisha yako.
1. Kuwa na routine ya kutunza ngozi yako yenye kueleweka. Routine ya kawaida huwa na cleansing (kuosha uso), Toning( kuweka uso sawa) na moisturizing ( kupaka mafuta) hizi unatakiwa kufanya kila siku kwenye ngozi yako yote. Tofauti ni kwamba mwilini hautatoni.
2. Kuondoa ngozi iliyokufa kwa kufanya scrub kwa wiki mara moja ndani ya miezi kadhaa kabla ya ndoa yako hii itafanya usiwe na kufanya haraka haraka ambayo haitaleta matokeo mazuri.
3. Facial and Hair Spa.
Hapa sasa anza kufanya facial na kwenda spa kwa ajili ya kutunza nywele zako. Kufanya hivi angalau kwa mwezi mara moja itakupa matokeo mazuri hata ile make up yako ambayo umebook kwa make up artist mkubwa na mtaalamu itakaa sawa kabisa siku ya harusi yako.
4. Clinical Sittings Na Homemade Treatments
Hapa sasa kama una makovu mengi mwilini na hutapenda yawepo hudhuria clinic za ngozi zenye kutoa huduma ya kuondoa madoa na makovu mwilini na uanze kufatiliza zile treatments za asili kama singo ya liwa na nyinginezo.
5. Mikono na miguu mizuri na Laini.
Anza kutumia mafuta ya alizeti kwa kufanya massage kwenye mikono na miguu yako kabla ya kulala hii itakupa matokeo mazuri zaidi.
6. Kutoa Nywele.
Hapa kwa wale wenye nywele nyingi za maeneo tofauti tofauti unaweza kufanya waxing katika spa na clinic tofauti tofauti kulingana na uwezo wako na ukubwa matokeo unayotaka.

7. Gym
Usitake crush results kwa kufanya crush diet ni bora usifanye crush diet, anza kuwa na healthy lifestyle kwa ajili yako. Fanya mazoezi na kujiweka fiti na ufanye jitihada kupata mwili kulingana na mahitaji yako na unavyotaka utokee siku yako ya harusi. Hii inaweza kuwa mwanzo mzuri wa wewe kuanza kuishi maisha yenye kuzingatia Afya yako kuanzia ndani hadi muonekano wako.
8. Jipe muda na kutafakari maisha yako na jee nini utaenda kuoffer kwa huyo unaeanza nae maisha pamoja. Kutafakari kutakufanya kukuondolea msongo wa mawazo unaoweza kusababishwa na mihemko ya siku hiyo.
9. Kula kwa afya na kunywa maji ya kutosha. Tajiri ni yule mwenye afya njema kwa kuwa ukiwa na afta njema utaweza kufanya chochote unachohitaji tofauti na ukiwa na maradhi. Hivyo basi zingatia ulaji wako.
10. Lala. Jitahidi upate muda wa kutosha wa kupumzika angalau masaa 6 hadi 8.
11. Massage.
Hii sio jambo la lazima sana ila kama utapenda kuondoa uchovu unaoletwa na maandalizi ya harusi basi hii ni muhimu sana kufanya. Jee ulikuwa unajua kupata massage kutoka kwa mtaalamu kwa lisaa limoja ni sawa na usingizi wa masaa 6 hadi 8. Massage ni moja ya njia nzuri ya kuondoa msongo wa mawazo na unaweza kujiskia vizuri siku nzima.
12. Kumaintain matokeo uliyoyapata.
Hapa kila bibi harusi anahisi kushindwa. Ni vizuri ukawa na njia ya kipekee itakayokusaidia kumaintain urembo na muonekano ulioutafuta kwa ajili ya siku yako ya harusi uendelee kuonekana vizuri.
Zingatia yale yanayofanya kazi kwako na uyafanye kwa bidii. Kila mmoja anahitaji muda kwa ajili yake maana ukijiskia vizuri unajiamini na unajipenda zaidi. Jipe muda kwa ajili yako.
Jee makala hii imekusaidia na umepata kujifunze chochote!?
Shea na uwapendao.
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Here you will find 68122 more Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kutunza-ngozi-kwa-bibi-harusi-mtarajiwa/ […]