SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna ya kutunza Ngozi Yenye Mafuta
Skin Care

Namna ya kutunza Ngozi Yenye Mafuta 

Faida kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi.

 Miongoni mwa mambo yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na hali isiyopendeza ni:-


1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya uvuguvugu na sabuni maalum Kitaalamu tunaita “cleanser” ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta. 

2. Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka, kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.


3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipoteze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea vichwa vyeusi (blackheads) 


4. Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi. 


5. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi na viambata sumu. 


6. Tumia maji ya vuguvugu wakati unaosha uso wako. 


7. Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe kupaka sabuni za kipande moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo kuziba.


8. Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa wiki.

Tunza ngozi yako ikutunze
©binturembo 

Related posts

4 Comments

 1. weed delivery toronto

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kutunza-ngozi-yenye-mafuta/ […]

 2. 다시보기티비

  … [Trackback]

  […] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kutunza-ngozi-yenye-mafuta/ […]

 3. Library

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kutunza-ngozi-yenye-mafuta/ […]

 4. 토렌트 사이트

  … [Trackback]

  […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/urembo/namna-ya-kutunza-ngozi-yenye-mafuta/ […]

Comments are closed.