SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kutunza Wig Lako
Urembo

Namna Ya Kutunza Wig Lako 

Nywele ni sehemu muhimu ya muonekano. Kiukweli nywele zinakamilisha muonekano . Nywele  zako zinaweza kufanya uonekane mdada wa maana au unalazimisha. Nakwambia nimeshaona wadada wamevaa kisista duu kweli ila nywele tu…nywele tu. Actually, hawa wadada ndio wamenimotivate hata kuandika hii article. Mara nyingi tunaassume watu hawaoni vitu. So tunatupia hatari, nguo kali, kiatu kikali alafu wigi kama nywele za mdoli uliosahaulika. People see, hata details ndogo. But kiukweli nywele ni detail kubwa sana. Iko juu ya kichwa na kitu cha kwanza mtu hutazama ni uso. Ukishatazama uso ukiinua jicho kidogo tu nywele hiyo. Kuna wigs mtu akivaa unaweza sema basi kapitiwa au style kakosea ila kuna nywele ukiziona unaona kutojali tu. Wig tulizozoea ni either human hair au synthetic. Personally nashauri mrembo awe na human hair hata kama ni kwa kuchanga taratibu sana. Lakini kama huwezi kuaffrord bado kuna namna unaweza kujali synthetic hair ikakaa vizuri. Warembo wengi wakijali sana wig zao utakuta wamepaka mafuta na kubrush tu, which is so wrong.  Nywele inahitaji matunzo. Hapa nimeweka namna ya kutunza human hair na synthetic hair kiujumla ili baada ya kupendeza na nguo zetu…nywele zisitulet down. Kuna matunzo ya ziada kwa baadhiya nywele lakini haya maelezo ni matunzo ya wigs kiujumla.

HUMAN HAIR 

Human hair wigs ni wig zilizotengenezwa na nywele halisi za biandamu. Mtu anaotesha nywele then anaikata na kuiuza kwa watengeneza wigi. Nywele hizi hutunzwa kama nywele halisi za mwanadamu. Kitu kimoja cha kunote ni kuwa mara nyingi nywele hizi huwa za watu wa asili nyingine (sio watu weusi) hivyo ni muhimu kujua namna ya kuzijali nywele hizi.

 Kuosha

Wig inapaswa kuosha ikiwa imesimama, isilowekewe  muda mrefu na si vyema kuvurugwavurugwa au kupikichwa kama nguo kwenye maji. Unaweza kuisimamisha kwa kuishika na mkono mmoja hata kama unaoshea dishi au kuiweka kwenye stand ili nywele zake zinyooke. Ni vyema zaidi kuosha wig kwa maji yanayotiririka badala ya maji kwenye chombo. Kabla ya kuosha hakikisha umebrush nywele zako, umezichana na kitana kikubwa au umelichambua na vidole ili kuachanisha nywele zilizofungana. Vitana vidogo huzivuta nywele kwenye wig na kuzikata. Osha wig lako na shampoo nzuri. Wig huchafuka na kunuka. Wakati mwingine products hubuild up na kufanya wig ipoteze nuru. Kuosha husaidia hata kustyle iwe rahisi. Usivae wig miezina halijagusa maji, litanuka. Ukikumbatiana na mtu anapokelewa na harufu mbaya.

Conditioner

Ni muhimu kuwa na conditioner. Kuwa na leave in conditioner na conditioner  ya kuosha. Kuwa na mazoea ya kulipaka wig lako conditioner. Conditioner hulainisha nywele, hung’arisha, huzichambua nywele na kuzuia kujifunga. Conditioner husaidia pia kurudisha na kufunga unyevunyevu ndani ya nywele. Conditioner ya kawaida hutumika zaidi wakati wa kuosha, na leave in hutumika kila siku wakati wa kustyle. Usispray kwenye kofia wala kwenye nywele za chini sana, conditioner hulainisha nywele hivyo inaweza kukata  nywele ikipuliziwa kwa chini sana. Unaweza kukuta wig safi ila limejifunga, nywele zimekuwa ngumu kama katani au kama nyuzinyuzi. Ukistyle likiwa hivi halitapendeza, tumia conditioner.

Kustyle

Human hair huimili vizuri moto hivyo unaweza kustyle human hair kwa pasi ya nywele (hair straightener) au curling iron. Pia unaweza kutumia rollers na kukausha kwa dryer ya mkono. Ukiwa na vifaa hivi itakuwa rahisi zaidi kustyle wig lako nyumbani. Kama hupendi au hauko vizuri katika kustyle wig lako basi peleka wig hilo salon kila linapohitaji huduma. Human hair wig inaweza kubadilishwa rangi kirahisi so unaweza kubadilishwa style kwa kupakwa rangi nyingine na pia kulikata

Kuhifadhi

Wig inapaswa kuhifadhiwa kwa kusimamishwa. Hii husaidia kutunza nywelw katika hali nzuri na kuzuia nywele kufungana. Kuna wig stands za bei ndogo sana siku hizi. Unaweza kununua hadi kwa 5000/= Kusimamisha wig huhakikisha style ya wig inakaa mahali pake kwa muda mrefu zaidi. 

SYNTHETIC HAIR

Synthetic hair ni nywele iliyotengenezwa na material tofauti na nywele za binadamu. Mara nyingi ni nyuzinyuzi zitokanazo na plastic. Synthetic hair mara nyingi huwa na gharama ndogo ukilinganisha na human hair. Mara nyingi nywele hizi huja na style ambayo hudumu muda mrefu sana na mara nyingi huwa ngumu kubadilisha. Synthetic hair nyingi haziwezi kubadilishwa rangi kirahisi maana hazikubali rangi za kawaida za nywele.

Kuosha

Usithubutu kuosha synthetic hair na maji ya moto sana kamwe. Unaweza kubadili wig lako from straight hair to afro.  Hii imenikumbusha kitu,Mama yangu anapenda sana usafi, wakati niko mdogo, mama wa watu aliamua kuosha wig zake kisawasawa. Lengo lake ni kuua bakteria na kuondoka mafuta yote kwenye wig zake. Baada ya maji kuchemka haswa aliyaweka kwenye beseni kisha kuloweka wig zake, enzi hizo hakuna human hair. Siku hiyo hizo wig zote zilirest in peace. Afro sio afro, dodoki sio dodoki. Please usioshe synthetic hair na maji ya moto. Synthetic haipatani na moto mkali, ni plastic. Osha na maji ya baridi yanayotiririka  likiwa limesimama. Kabla ya kuosha chana na kitana kikubwa na chambua nywele zilizofungana na vidole. Osha wig lako na shampoo nzuri kuondoa harufu, uchafu na bidhaa za nywele zilizoganda.

Conditioner 

Ni muhimu sana kuwa na conditioner mbili. Baada ya kuosha wig lipake conditioner kisha acha kwa dakika tatu alafu suuza na maji yanayotirirka. Wakati unaosha usichane wig na kitana kidogo, lichambue na vidole. Usilipanguse sana, liguse taratibu na taulo kama unalikanda. Lining’inize likauke likiwa limesimama wima. Jitahidi kulipulizia conditioner kila unapovaa, synthetic wigs uwahi kupoteza unyevunyevu. Synthetic hair huwa na leave in conditioner zake maalumu.Fabric softener ni conditioner nzuri kwa synthetic hair pia, changanya nusu fabric softener na maji nusu. Spray mchanganyiko huu kwenye wig lako. Usispray kwenye kofia wala kwenye nywele za chini sana, conditioner hulainisha nywele hivyo inaweza kukata  nywele ikipuliziwa kwa chini sana.

Kustyle

Synthetic hair ni plastic, plastic haipatani na moto mkali isipokuwa heat resistant synthetic hair ambazo huandikwa kwenye kifungashio chake. Mara nyingi synthetic hair huja na mtindo ambayo si rahisi kubadilisha lakini baada ya kuosha na conditioner nywele hulaa vizuri yenyewe.Ili kuongeza curls unaweza kutumia rollers na maji ya moto kiasi. Baada ya kuweka rollers kwenye wig lako dumbukiza kwenye maji ya moto kiasi kwa dakika chache sana kisha litoe na acha likauke. YouTube kuna video kadhaa za namna ya kustyle synthetic hair. Hakikisha unalispray wig lako na hair spray baada ya conditioner. Kuna spray maalumu za synthetic hair, unaweza kutumia spray za rasta. Kwa heat resistant hair unaweza kutumia vifaa vya moto kustyle lakini si vyema kuvitumia mara kwa mara.

Kuhifadhi

Kama ilivyo katika human hair, hifashi synthetic hair kwa kuzisimamisha. Synthetic hair hujifungafunga kwa urahisi sana hivyo sio vyema kulikunja kwa namna yoyote wakati wa kulihifadhi.

I hope hizi tips zimekusaidia kukupa muongozo wa kuanza kujali wig zako. Ni vyema kufatilia tutorials mbalimbali juu ya matunzo ya mawig ili ufahamu mengi zaidi. Kumbuka unaweza pia kupeleka wig lako salon likafanyiwa huduma badala ya kufanya hatua zote mwenyewe. Cha msingi ni kuwa na conditioner, hair spray na chanuo au brush sahihi kwa ajili ya kuliweka  wig lako sawa kidogo kila unapolivaa.

Imeandikwa na @elegancebyRee

Related posts