SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

NATURAL WAYS ZA KUONDOA MADOA YALIYO TOKANA NA CHUNUSI
Skin Care

NATURAL WAYS ZA KUONDOA MADOA YALIYO TOKANA NA CHUNUSI 

Well wengi wetu tuna zile dark spot zilizo tokana na chunusi eidha kwa kutumbuliwa au kuto kutumbuliwa chunusi ikiisha inaacha alama au doa jeusi.

lakini kabla ya kukupeleka kwenye matibabu kwanza tukwambie jinsi ambavyo una weza kuepukana na tatizo hili la madoa usoni

1) usitumbue /  kuchezea kipele chako

iweke mikono yako mbali na kipele chako unapo kitumbua una paka kidonda na bakteria wana ingia hili kidonda kipone ni lazima ile ngozi ngumu ijifunge kwa juu na hakuna anae penda ile situation unapo itoa ile ngozi ngumu una baki la laini lakini yenye doa.

2) epuka jua

lile doa lilnalo baki lina weza kuji safisha lenyewe likaja kwenye hali yake ya kawaida endapo tu uta li treat vizuri kwa kuto kuexpose kidonda chako juani, ila kama jua litakua rafiki yako basi litasababisha lile eneo kuzidi kuwa jeusi.

NJIA ZA KUONDOA WEUSI ULIOTOKANA NA CHUNUSI

  • Maji Ya Limao

Lemon-juice-for-bleaching-dark-skin-spots-and-acne-scars

limao husifika kuwa na acid ambayo ina safisha ngozi haraka, sio tu kusafisha bali ina weza kuondoa kabisa madoa katika ngozi, limao ni jibu zuri katika matibabu mbali mbali ya ngozi kama una chunusi pia husaidia kuondoa,

i)una weza kutumia maji ya limao kwa kukamua maji ya limao na kutumia pamba au vidole kupaka sehemu iliyo athirika kaa nayo kwa dakika kumi kisha ondoa na maji masafi, fanya hivi kwa muda wa week mbili utapata matokeo

ii) kama una ngozi sensitive dilute maji ya limao kwa ku mix na rose water halafu fanya process kama ya kwanza hapo juu

  • Asali

honey-e1474216803723

i)paka asali kwenye doa iache kwa usiku mzima osha uso wako asubuhi

ii) changanya asali vijiko viwili , aspirin 2-3 na maji kidogo – weka maji kidogo kisha tumbukiza aspirin zako changanya mpaka upate uji uji wa aspirin halafu changanya na asali ipake katika sehemu iliyo athirika na uache kwa dakika 15 kisha ifute.

 

  • Aloe Vera

Can-Aloe-Vera-Heal-Acne-Scars-Other-Skin-Benefits-770x402

Aloe Vera  sio ina uwezo wa kufanya ngozi yako iwe soft bali pia ina uwezo wa ku- regenerate damaged tissue na ku boost healing process ni nzuri sana kama itatumiwa ikiwa fresh kutoka kwenye mti

i) chukua jani la mu aloe vera na likate upate ule uteute mweupe ndani, paka ule ute katika sehemu iliyo athirika halafu iache kwa dakika 30. Fanya hivi mara mbili kila siku ili upate matokeo mazuri. sio tu ita safisha sehemu iliyo athirika bali itakupa ngozi nyororo.

  • olive oil

Olive-Oil-helps-in-getting-rid-of-acne-scars

olive oil ina semakani ni rafiki wa ngozi sababu ina vitamin A, D, E, C, B1 na  B2 pia ina iron na antioxidants ambazo zina weza kusaidia kuondoa madoa usoni

i)chukua olive oil na paka taratibu usoni massage uso wako taratibu na focus zaidi kwenye sehemu zilizo athiriwa (zenye madoa), massage kwa muda mpaka pale utakao ona ngozi imenyonya mafuta kisha chukua maji ya uvugu vugu na tumbukiza taulo au nguo yoyote katika maji hayo weka usoni kwa dakika chache usijifute, baada ya hapo osha uso wako kwa maji ya kawaida.

  • Baking Soda

bakingsodawater

chukua vijiko kadhaa vya baking soda mix na maji, ukisha pata ule uji uji paka kwenye sehemu yenye doa, massage sehemu hio kwa dakika 2-3 kisha acha uji huo ukae kwa dakika chache, osha uso wako na paka mafuta (mazuri zaidi ni olive oil) fanya hivi mara mbili au tatu kwa week.

 

Related posts