SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Nazi Inavyoweza Kukupa Ngozi Nyororo
Skin Care

Nazi Inavyoweza Kukupa Ngozi Nyororo 

Hivi unajua kuwa unaweza kuwa mrembo kwa kutumia vitu vya asili tu?. Ndio inawezekana!. Wengi wetu tumekariri kwamba, ili uwe mrembo na mwenye muonekano wa kuvutia machoni pa watu, basi ni lazima utumie vipodozi vya madukani, vyenye kemikali za sumu. Na vipodozi hivi vinauzwa kwa bei ghali kweli. Na wakati mwingine usipate hata matokeo uliyokuwa unategemea. Unakuwa umepoteza pesa na umezidi kuharibu muonekano wako wa asili.

Leo fahamu maajabu ya nazi katika urembo.  Tumezoea kutumia nazi jikoni kwenye mapishi, lakini nazi pia inaweza ikatumika kama scrub ya ngozi yako.

Fuata hatua hizi hapa chini ili kufanya ngozi ya uso wako iwe laini, nyororo na kufanya uso wako  wenye mvuto. Scrub hii unaweza pia kuitumia kwa mwili mzima, lakini kwa leo nitaelezea namna ya kutumia kwa uso wako.

NINI CHA KUFANYA:
1. Andaa nazi yako kwa kuikuna vizuri na ili upate matokeo mazuri jitahidi kuikuna taratibu ili itoke laini.
2. Safisha uso wako kwa maji safi na sabuni ya kawaida isiwe sabuni ya dawa (medicated)
3. Kausha uso wako kwa taulo safi.

4. Baada ya uso wako kuwa mkavu, ichukue ile nazi yako uliyoikuna tayari, taratibu anza kusungua usonio kwa dakika kama 3 mpaka 5.

5. Ukishamaliza hapo, utakaa hivyo bila kuuosha uso wako kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.
6. Baada ya muda huo, utaosha uso wako kwa sabuni ya kawaida.

7. Kausha uso wako kwa taulo safi, kisha paka losheni yako unayotumia siku zote.

Kupata matokeo mazuri Fanya Mara mbili kwa wiki. 

Tahadhari : Kama una Ngozi ya mafuta usifanye hii! Itaongeza mafuta zaidi, na utazidisha chunusi zako. Pata ushauri Kwanza kutoka kwa mtaalamu. 
Shea na uwapendao
Imeandikwa na @binturembo

Related posts