SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Ng’arisha Ngozi Kwa Kutumia Unga Wa Dengu
Dondoo

Ng’arisha Ngozi Kwa Kutumia Unga Wa Dengu 

Unaweza ukawa una penda kupika/kula bagia za dengu au chakula chochote kinacho pikwa kutokana na unga wa dengu bila kujua unaweza kutumia dengu hio hio katika kufanya ngozi yako ing’ae. Kama ambavyo binadamu tunategemeana na mimea na wanyama katika kupata mahitaji yetu basi ndivyo ilivyo katika mahitaji ya jikoni na urembo na afya, kuna vyakula ambavyo unaweza ukala lakini pia unaweza kutumia katika urembo.

Chickpea Flour in a bowl

Leo tunakupa tips chache za namna unavyo weza kutumia unga wa dengu kung’arisha ngozi yako.

Mahitaji

  • Unga wa dengu vijiko viwili vya chai
  • Yai moja la kienyeji
  • limao

Namna ya kuandaa

Weka unga wa dengu katika kibakuli au chombo kisafi, kisha vunja yai pembeni na utoe kiini ambacho utakichanganya na unga.

Koroga mpaka uhakikishe mchanganyiko huo umechanganyika na kulainika kabisa.

Baada ya hapo safisha uso wako kwa maji ya uvuguvugu kisha jikaushe kwa taulo au kitambaa kisafi.

Baada ya kuhakikisha uso wako uko safi paka mchanganyiko huo kwa kuusambaza uso mzima, ikiwezekana pia katika maeneo ya shingoni na pembezoni mwa masikio ili kuzifanya pia sehemu hizo kuwa zenye mvuto wa aina yake.

Kaa na mchanganyiko huo kwa dk-15 kisha futa/osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu.

Namna Nyingine #2 

Mahitaji 

  • Vijiko Vinne Vya Unga wa dengu
  • Limao kijiko kimoja
  • maziwa kijiko kimoja

Namna ya kuandaa

Changanya unga, maziwa na limao kisha paka usoni mwako au sehemu yoyote ambayo ungependa kung’arisha, massage hio sehemu kwa dakika kadhaa kisha acha mchaganyiko huo katika uso wako mpaka ukauke.

Ikisha kauka osha kwa maji ya vuguvugu.

Ukitumia na ukipata matokeo usisite kutujulisha.

 

Related posts

4 Comments

  1. wonka bar

    … [Trackback]

    […] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/ngarisha-ngozi-kwa-kutumia-unga-wa-dengu/ […]

  2. 소액결제

    … [Trackback]

    […] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/ngarisha-ngozi-kwa-kutumia-unga-wa-dengu/ […]

  3. 티비위키

    … [Trackback]

    […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/ngarisha-ngozi-kwa-kutumia-unga-wa-dengu/ […]

  4. Buy Polka Dot Mushroom Bars online with prescription

    … [Trackback]

    […] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/urembo/ngarisha-ngozi-kwa-kutumia-unga-wa-dengu/ […]

Leave a Reply