SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Ng’arisha Ngozi Kwa Maji Ya Mchele
Skin Care

Ng’arisha Ngozi Kwa Maji Ya Mchele 

Kuna vitu unaweza kuvisikia na usiamini lakini ni kwamba maji ya mchele yanaweza kukupatia ngozi nyororo na ng’avu, maji ya mchele ni siri ya urembo kwa wanawake wa ki-Japanese, tulishawahi kuona namna wanatumia maji ya mchele kukuza nywele lakini kumbe inawezekana kutumia hata katika ngozi, badala ya kutumia bidhaa zenye kemikali wao hutumia maji ya mchele katika ngozi na nywele zao.

Faida Za Maji Ya Mchele Katika Ngozi 

  • maji ya mchele yanaweza kutumika katika aina zote za ngozi kama ngozi kavu na ngozi yenye mafuta
  • Maji ya mchele yana vitamini kama vile B1, C, E, pamoja na madini, ambayo yanaweza kupunguza matobo katika ngozi, kukaza ngozi, kupunguza mistari ya uzee na pia kuang’aza ngozi yako.

  • Maji ya mchele pia husaidia kuponya chunusi na hupunguza wekundu katika ngozi.  inaimarisha ngozi na kuifanya iwe nyororo na kuipa ugumu.

Namna Ya Kutengeneza Maji Ya Mchele

 safisha mchele kwa kutumia maji ili kuondoa uchafu au uchafu wowote. Weka mchele katika bakuli miminia maji. loweka mchele wako kwa dakika 30, kisha toa mchele katika maji hayo na mimina maji yako katika chombo safi na maji yako ya mchele yatakuwa tayari kwa matumizi

Namna Ya Kutumia Maji Haya Kung’aza na Kusafisha Uso

  • Jinyunyuzie maji ya mchele kidogo katika uso wako na taratibu massage uso wako kwa dakika moja, baada ya hapo osha uso wako kama kawaida na utaanza kuona matokeo katika ngozi yako, fanya hivi kabla ya kwenda kuoga. unaweza kuhifadhi maji yako katika kikopo chenye mfuniko, unaweza kuyatumia kwa siku 5 baada ya siku hizo tengeneza mengine.

 

Kuna namna tofauti za kung’aza ngozi yako kwa asili unaweza ku click hapa kusoma lakini pia ukijaribu husisite kutupa matokeo katika mitandao yetu ya kijamii.

Related posts

2 Comments

  1. rich89bet

    … [Trackback]

    […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/urembo/ngarisha-ngozi-kwa-maji-ya-mchele/ […]

  2. pics of liberty cap mushrooms

    … [Trackback]

    […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/ngarisha-ngozi-kwa-maji-ya-mchele/ […]

Comments are closed.