Siku chache zilizo pita tuliuliza hili swali katika kurasa yetu ya Instagram ambapo watu wengi walijitokeza kujibu, kwanini tuliuliza? kwasababu sikuhizi tunawaona wadada/wamama wanabeba handbag kubwa na nzito mno hii ilitufnye tuwaze nini kipo katika handbags zao na amini usiamini huwa kuna vitu vingi mno vinabebwa kwa maana vilitajwa vitu vingi hadi tukawaza ni kweli mtu anatumia hivyo vitu vyote kila siku day in day out? au ndio ule uvivu wa kuvitoa na kuvirudishia kila mara? kwetu sisi tuna hisi inapaswa wanawake wakawa na ratiba ya kubeba vitu kwenye handbag zao, pale kitu kinapo hitajika kubeba basi ni vyema kikabebwa lakini kama si lazima kubebwa kwa siku hio basi kiachwe tu hadi pale kitakapo kuwa na uhitaji. Leo tunawaletea vile ambavyo ni muhimu kuwa navyo kila siku na vimetajwa kwa wingi katika post yetu.
- Wallet – ni muhimu katika kuhifadhi vitu vidogo vidogo kama pesa, vitambulisho, card za bank, picha nakadhalika hii inakufanya uwe na vitu muhimu katika sehemu moja na kujua kipi ukipate wapi na pia inapunguza mzigo katika hanbag yako
- Khanga/mtandio – kama mwanamke/msichana nimuhimu kubeba khanga katika mkoba wako hujui nini kitatokea saa ngapi na wapi, nguo inaweza kuchanika ukajistiri kutumia khaga/mtandio wako.
- makeup bag – makeup bag inasaidia kuweka makeup zakona vitu vyako vya urembo kama perfume, nail cutter, lip balms, lipstick, wipes,pads, makeups etc hii pia inakupa urahisi wa kubeba vitu vichache make up bags huwa ndogo fulani kuliko kutupia vitu tu kwenye handbag unaweza ukajikuta una hamishia dressing table nzima kwenye handbag lakini ukiwa na makeup bag unakuwa limited na unaanza kuchagua kipi muhimu kuwa nacho na kipi si cha muhimu.
- note book ,pen,kitabu – hivi vitakusaidia katika kutengeneza to do list yako ya siku hio, kuwa na planned day saa ngapi ufanye nini nakadhalika.
kwetu hivyo ndivyo tulivyo viona ni muhimu kuwa navyo huitaji handbag kubwa au handbag iwe nzito kwa kubeba vitu ambavyo huna umuhimu navyo kila siku NOTE: ni vizuri kuwa unaangalia handbag yako mara kwa mara kubadilisha vitu vilivyopo ndani ya handbag yako kutokana na mahitaji yako.
Related posts
4 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] There you will find 90911 more Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/nini-kipo-katika-handbag-yako/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/urembo/nini-kipo-katika-handbag-yako/ […]
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/nini-kipo-katika-handbag-yako/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/nini-kipo-katika-handbag-yako/ […]