SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

NINI ULE KUIPA NGOZI AFYA
Afya

NINI ULE KUIPA NGOZI AFYA 

Wote tunapenda kuonekana warembo na vijana. Lakini inawezekana ukawa unajiharibu zaidi katika kujifanya uwe mrembo leo na kujiletea madhara makubwa yasiyotibika kesho. Pia, inawezekana unatumia hela nyingi na muda mwingi katika kuhakikisha ngozi yako inakuwa nyororo, nzuri, na ya kuvutia. Je, unafahamu kuwa kuna aina za vyakula vinavyosaidia katika kutunza ngozi yako?

Kama ambavyo unajitahidi kufuata kanuni za afya ili kuufanya mwili wako uwe vizuri – chakula bora, mazoezi mara kwa mara, kupumzika kwa muda mrefu – vivyo hivyo ngozi yako inatakiwa kutunzwa kutokana na kanuni asilia. Hapa tunakuletea vyakula vinavyotunza ngozi yako bila gharama yeyote.

MBOGA ZA MAJANI

arthritis2Mboga za majani zina vitamini A nyingi sana. Vitamin A ni muhimu kwenye ngozi sababu ndio kitu kikubwa kwenye kusaidia ngozi kuzalisha seli mpya na kuondoa zile zilizokufa, hivyo kupunguza ukavu na kutunza ngozi na kuifanya kungara na kuvutia.

MATUNDA

 

citrus-fruits

Matunda yenye vitamin C – chungwa, limao na mengine mengi – ni muhimu kwa afya ya ngozi yako sababu inasaida kutengeneza collagen, aina ya protini inayotengeneza ngozi.

Vitamin C inasaidia kuondoa uvimbe na mikunjo ya ngozi hivyo kuilinda ngozi yako kuzeeka mapema.

ASALI

honeyjar

Asali ni afya kwa binadamu, hutengenezwa na nyuki kwa viambato asilia. Chochote kile ambacho ni kizuri kwa afya yako ni nzuri kwa ngozi pia. Ngozi yenye afya inatakiwa kuhifadhi unyevunyevu ili kuzuia kukauka na kupasuka. Hii ndio sababu kubwa ya kutumia mafuta ili kuweka ngozi iwe na unyevunyevu. Asali husaidia kuleta na kuhifadhi unyevunyevu kwenye ngozi.

Ili kuweza kulinda ngozi, paka asali wakati wa kuoga, acha kwa muda kisha ioshe. Ni zoezi la muda mfupi linalohakikisha ngozi yako inanawiri vizuri.

Asali ina kiwango kikubwa cha sukari na asidi ambavyo huzuia vijidudu (Bacteria) wanaozaliana kwenye ngozi.

Related posts

2 Comments

  1. More Bonuses

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/urembo/nini-ule-kuipa-ngozi-afya/ […]

  2. weed delivery toronto

    … [Trackback]

    […] There you will find 92833 additional Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/nini-ule-kuipa-ngozi-afya/ […]

Leave a Reply