SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Njia 3 Za Kusafisha Accessories Zako Za SIlver
Urembo

Njia 3 Za Kusafisha Accessories Zako Za SIlver 

Dhahabu inaweza ikawa ni rafiki wa karibu wa mwanamke lakini silver ni rafiki tegemezi kwa mwanamke, acccessories za silver ndizo huvaliwa sana na mwanamke na zinafanya mtoko wako upendeze zaidi zinaweza kufanya mtoko wako ushine na zinaendana na rangi nyingi za nguo. Pia ni rahisi kununua accessories za silver kuliko dhahabu.

Lakini ni vito ambavyo vinachafuka sana unaweza husivitamani wala kuvitaka tena vikichafuka well tunakupa tips za nini unaweza kufanya vito vyako hivi vikichafuka

  • loweka katika foil

aluminium foil ikichanganywa na chumvi inaweza kusafisha vito vyako vizuri zaidi,weka aluminum foil katika bakuli au kikombe chako, mimina maji ya moto na weka chumvi yako kisha ingiza accessories zako katika mchanganyiko huo na uache kwa dakika 10-15, utaona jinsi ambavyo uchafu unatoka na vito vyako vina rudi katika hali yake ya ung’avu vitoe na uache vikauke.

  • Loeka kwa muda mrefu

Njia nyingine ya kusafisha vito vyako vya silver ni kwa kuviloeka kwa muda, unaweza kuloeka na sabuni ya unga, baking soda na limao au ndimu, unaweza kuviloeka kwa siku nzima au masaa kadhaa na kuvitoa vikauke, you will amezed on how this tricky can work wonders.

  • Dawa Ya Mswaki

Kama vito vyako ni vya bei ghali ni vyema ukaenda kwa sonara au kununua dawa za kusafishia vituo, lakini kama ni vya bei rahisi basi jibu lako ni dawa ya mswaki, chukua dawa ya mswaki weka kwenye chombo changanya na maji na baking soda kidogo, kisha tumia mswaki kusafishia vito vyako, chukua mswaki ambao ni mlaini ilikuepuka kuchuna vito vyako.

Kujua namna ambavyo unaweza kutunza wig lako,bonyeza hapa

Related posts