SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Njia 7 Za Kupunguza Kitambi Haraka
Urembo

Njia 7 Za Kupunguza Kitambi Haraka 

Kupunguza kitambi/tumbo ni changamoto kubwa ni kitu ambacho kina tunyima amani wengi lakini namna ya kukipunguza huwa ni ngumu sana, wengi huwa tuna fanya diet au kuamua kwenda gym kweli zina weza kusaidia lakini kama huwezi hivyo vyote ni nini ufanye?

 1. Kunywa Maji

mara nyingi huwa tunakua wavivu kunywa maji, lakini ukijiwekea kuwa una kunywa maji mengi/mara kwa mara kwa siku itakusaidia kuto kusikia njaa, hii itakufanya uwe mbali na vyakula vyakula vya hapa na pale visivyo kuwa na msingi lakini pia maji yana saidia kufanya ngozi iwe nyororo so ni maji maji maji maji. unaweza kuongezea vitu kama limao, tango, tangawizi katika maji yako inaitwa detox water

2.Pata Usingizi wa kutosha

hii itakuepusha na kutaka kula chakula usiku sana, unapo wahi kulala unawahi kula hii inasaidia mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi yake vizuri.

3.Punguza/Acha Kunywa Soda

Sukari ni moja ya vitu vibaya vinavyo anzisha/kuleta unene kaa mbali nazo na anza kunywa maji kwa wingi, fresh juice na green tea husaidia sana kupunguza hamu ya kunywa soda lakini pia hazileti negative effects katika mwili wako tofauti na soda

4.Weka Ratiba Ya Chakula

ni vizuri kama utakuwa unajipikia mwenyewe maana utajua uweke chumvi, sukari kiasi gani, mafuta nk. Pangilia ratiba yako ya week nzima lakini pia katika ratiba yako weka healthy food ambazo zitakufanya uweze kupuguza mafuta mwilini,

5.Acha Kula VitaFunwa Vidogo Dogo

biscuits, Big G, Chocolate ni vitamu na vina temptation sana lakini navyo vinaongeza sukari na kusababisha kuleta unene tumboni jaribu kuviepuka sana tembea na fresh juice, unapo jisikia kula kitu kitamu kitamu kunywa juice.

6.Kula taratibu – yes hili huwa tunalishindwa sana, lakini kula taratibu kuna saidia kumeng’enya chakula chako vizuri lakini pia kunafanya ule chakula kidogo na kushiba haraka.

7.Mafuta si rafiki yako – mafuta ni mabya sana katika chakula jaribu kutumia mafuta yenye less cholesterol, kama mafuta ya nazi, olive oil, almond au pika chukuchuku ukiongezea chakula chako na parachichi, parachichi linaweza kusababisha chakula kiwe kitamu na lina mafuta ambayo hayana madhara

Related posts

2 Comments

 1. 다시보기사이트

  … [Trackback]

  […] There you can find 88275 additional Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-7-za-kupunguza-kitambi-haraka/ […]

 2. สล็อต ฝากถอน true wallet เว็บตรง 888pg

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-7-za-kupunguza-kitambi-haraka/ […]

Leave a Reply