SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Njia Asili Za Kuondoa Utofauti Wa Rangi Ya Ngozi Unaosababishwa Na Mionzi Ya Jua
Skin Care

Njia Asili Za Kuondoa Utofauti Wa Rangi Ya Ngozi Unaosababishwa Na Mionzi Ya Jua 

Katika shughuli za kila siku swala la miili yetu kupatwa na mionzi ya jua limekuwa jambo la kawaida. Mionzi hii sio tu huifikia ngozi zetu lakini pia huweza kusababisha mabadiliko fulani katika ngozi kupelekea zionekane zimefifia au nyeusi zaidi. Mfano mzuri mtu akitembea juani kwa muda mrefu utaona rangi ya paji la uso liko tofauti na sehemu nyingine za uso au kwa wale wenzetu wanaovaa nguo zinazoacha wazi maeneo ya kifua au mgongo utagundua rangi za maeneo hayo iko tofauti na sehemu zingine za mwili. Hali hii inajulikana kama suntanning. Hutokea pale ngozi inapozalisha zaidi chembe hai zinazofanya kuwa na rangi nyeusi (melanin), ikijaribu kujilinda dhidi ya uharibifu unaoweza kusababishwa na mionzi ya jua. Leo nimekuandalia njia za asili na rahisi ambazo unaweza kuzitumia ili  kusaidia kuondoa utofauti wa rangi ya ngozi unaoletwa na mionzi ya jua.

1. Nyanya na Asali.

Mahitaji:- nyanya kubwa 1 na asali (kijiko kikubwa)

Namma ya kufanya:-kuna njia mbili unazoweza kutumia kuandaa remedy hii. (i) chukua nyanya, ikate katikati na uchovye asali upande huo ulioukata kisha anza kupaka sehemu husika.

Au (ii) Chukua nyanya uisage na kisha changanya asali na uanze kupaka. Subiri kwa dakika 15 hadi 20 baada ya hapo nawa maji halafu jikaushe kwa kitambaa safi. Fanya hivi kila siku kupata matokeo yanayo ridhisha.

2. Tango na Asali.

Mahitaji :-

  • Tango 1,
  • Asali (kijiko 1 cha chai).

Namna ya kufanya:- Saga tango kisha changanya na asali. Paka mchanganyiko huu sehemu iliyoathiriwa, subiri kwa dakika 10 hadi 15 kisha nawa maji. Tumia njia hii mara moja au mbili kila siku.

3. Limao na sukari.


Mahitaji:-

  • Limao
  • sukari (kijiko kikubwa 1)

Namna ya kufanya:- Kamua limao kupata maji yake kiwango cha kijiko 1 na uchangaje sukari kwenye maji ya limao. Tumia mchanganyiko huu kama scrub katika sehemu iliyoathiriwa kwa ku massage taratibu kwa dakika 2 hadi 3 kisha nawa na maji. Fanya hivi mara kwa mara kupata matokea mazuri zaidi.

4. Apple cider vinega na Baking soda.


Mahitaji:-

  • Baking soda (kijiko 1 cha chai)
  • vinega (kijiko 1)

Namna ya kufanya:- Changanya baking soda na vinega kupata mchanganyiko ambao sio mzito sana. Paka mchanganyiko huu kama scrub na subiri kwa dakika 5 hadi 10 halafu unawe. Tumia hii mara moja au mbili kwa wiki.

5. Papai

Mahitaji:-

  • Papai lililoiva.

Namna ta kufanya:-  Chukua papai menya halafu ulisage. Paka mchanginyo huu sehemu husika na usubiri kwa dakika 15 hadi 20 kisha nawa kwa maji ya uvugu uvugu. Paka kila siku au mara kwa mara mpaka utakapopata matokeo yatakayo kuridhisha.

6. Kiazi mviringo.


Mahitaji:-

  • Kiazi mviringo 1.

Namna ya kufanya:- kata kiazi katikati, kisha anza kusugua sehemu husika taratibu.

Mbali na njia hizi zilizotajwa, pia inashauriwa kutumia mafuta maalum (sunscreen) ili kuikinga ngozi kutokana na madhara ya mionzi ya jua. Kama una maswali zaidi au maoni kuhusina na mada hii, tunakukaribisha kukomenti hapo chini.

Instagram @gift_reinhard

Related posts

4 Comments

  1. check this site out

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-asili-za-kuondoa-utofauti-wa-rangi-ya-ngozi-unaosababishwa-na-mionzi-ya-jua/ […]

  2. can you buy psilocybin in denver,

    … [Trackback]

    […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-asili-za-kuondoa-utofauti-wa-rangi-ya-ngozi-unaosababishwa-na-mionzi-ya-jua/ […]

  3. weed delivery toronto

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-asili-za-kuondoa-utofauti-wa-rangi-ya-ngozi-unaosababishwa-na-mionzi-ya-jua/ […]

  4. saxenda weight loss

    … [Trackback]

    […] Read More here on that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-asili-za-kuondoa-utofauti-wa-rangi-ya-ngozi-unaosababishwa-na-mionzi-ya-jua/ […]

Comments are closed.