SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Njia Za Kuondoa Weusi Shingoni
Urembo

Njia Za Kuondoa Weusi Shingoni 

Kuwa na rangi tofauti shingoni na mwilini huwa inakera unaonekana mchafu, hata kama una rangi au ngozi nzuri sehemu nyingine lakini ukiwa na shingo nyeusi huwa inaleta picha mbaya. Shingo nyeusi hutokana na kuisahau, unaweza kukuta tunafanya kila nyia kuwa na ngozi nyororo usoni na sehemu nyingine za mwili lakini tunasahau kabisa shingo. Kuna wengine hata mafuta hawapaki shingoni.

Leo tunakuletea njia chache ambazo unaweza kutumia katika kuondoa weusi huu.

  • Apple Cider Vinegar

Apple Cider Vinegar husaidia kuzawazisha kiwango cha pH cha ngozi, husaidia kukupa mng’ao wa asili lakini pia huondoa seli za ngozi zilizokufa. Uwepo wa asidi ya malic katika ACV hufanya iwe exfoliator nzuri.

Unachohitaji kufanya ni kuchukua vijiko 2 vya siki ya apple cider na vijiko 4 vya maji na uchanganye vizuri. Paka mchanganyiko huu katika shingo yako na kaa nao kwa dakika 10 kisha unaweza kuosha kwa maji au ukaenda kuoga. Fanya hivi mara kwa mara ili kupata matokeo ya haraka

Note: Hakikisha una moisturizer ngozi yako mara tu ukimaliza kuosha ngozi yako ya ngozi kwa sababu ACV husababisha ngozi kuwa kavu.

  • Baking Soda 

Baking Soda inasaidia pia katika kuondoa seli za ngozi zilizokufa, kuleta mg’ao lakini pia husadia katika ku-promote circulation

Chukua vijiko 2/3 vya baking soda na maji ya kutosha au limao kutengeneza smooth paste. Paka mchanganyiko wako katika shingo na uache ukauke, ukisha kauka ondoa/bandua mchanganyiko huu kwa kutumia vidole vyako (viloweshe ili usipate maumivu wakati wa kuondoa). Kisha unaweza kuosha kwa maji na kupaka mafuta yako, fanya hivi kila siku ili kupata matokeo kwa haraka.

  • Juice Ya Viazi

Kiazi kinasemekana kuwa na bleaching proprieties mbayo inaweza kurahisisha ngozi kwa kiwango kikubwa. Pia husaidia kuondoa weusi katika ngozi yako na kukufanya uwe na rangi moja katika ngozi.

Chukua viazi na upondeponde ukishapata uji wa viazi kamua na chuja ili kupata juice nyepesi, paka kwenye shingo yako na uache ikauke, ikishakauka unaweza kuosha kwa maji ya uvuguvugu. Fanya hivi mara mbili kwa siku kupata matokeo kwa haraka.

  • Mtindi

Mtindi una nzymes asili ambayo husadiana na asidi ambayoipo katika limao kutoa matokeo yanayohitajika. Inang’alisha zaidi ngozi na kuifanya iwe laini.

bowl and spoon with joghurt

Chukua vijiko 2 vya mtindi na kijiko cha maji ya limao. Changanya viungo hivi viwili na utumie /paka mchanganyiko huu kwenye shingo. Acha kwa muda wa dakika 20 kabla ya kuosha na maji

Related posts

5 Comments

  1. mario 1 up mushroom

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-za-kuondoa-weusi-shingoni/ […]

  2. where to order Blue Foot magic Mushroom for sale online near me

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-za-kuondoa-weusi-shingoni/ […]

  3. best way to make passive income

    … [Trackback]

    […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-za-kuondoa-weusi-shingoni/ […]

  4. 뉴토끼

    … [Trackback]

    […] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-za-kuondoa-weusi-shingoni/ […]

  5. 호두코믹스

    … [Trackback]

    […] Here you can find 42944 additional Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-za-kuondoa-weusi-shingoni/ […]

Comments are closed.