SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Njia Za Kutunza Nywele Wakati Unanyonyesha
Urembo

Njia Za Kutunza Nywele Wakati Unanyonyesha 

Wanawake wengi wanakuza nywele zao vizuri kipindi cha ujauzito na zinakua vizuri lakini mara baada ya kujifungua nywele zinakatika hasa katika kingo za mbele (edges) hii ni kama desturi, Na kuzikuza kurudi zilivyokuwa huwa inachukua muda kidogo, lakini kuna namna ambavyo unaweza kutunza/kujali nywele zako ukaweza kukonyesha na nywele zako zikiwa katika hali nzuri tu.

  • Kuwa Muangaliafu na uchaguzi wa Shampoo – Chagua shampoo ambazo zinajaza nywele kuliko zile conditioning shampoo, sababu conditioning shampoo nyingi zina chemical ambazo zina punguza uzito wa nywele zako kwa ajili ya muonekano mzuri kupunguza ujazo wa nywele.

  • Chagua Conditioner inayofaa – chaagua conditioner zilizo tengenezwa kwa nywele nyepesi hizi nyingi huwa zina tengenezwa na viungo vya kuongeza uzito nywele hii itakusaidia kujaza nywele zako.

 

  • Protective hair styles – ni vyema ukasuka misuko inayo kinga nywele zako na kukatika, misuko kama yeboyebo, sangita etc ile ambayo ukifumua unaweza kuchomoka nywele achana nayo zitakatika maradufu badala ya kuziongeza.unaweza kusuka njia tatu, mabutu nk.

  • Tunza Afya Ya Mwili Wako -wanasema “a healthy body equals to healthy hair” kula vizuri,fanya mazoezi, usisahau kula vitamins hii haita saidia tu kujaza nywele zako bila kuwa fit mom na kupata beautiful skin.

 

  • Tunza Nywele Zako Kama Unavyo Tunza Brazilian Weave Yako – tumia wide tooth comb,epuka kuchana nywele wakati zimeloa, ikiwezekana epuka kuweka dawa (relaxing) na kupaka rangi nywele katika kipindi hiki.

ni matumani yetu dondoo hizi zitakusaidia, ukipenda kujua namna ya kutunza nywele kavu bonyeza hapa

Related posts

1 Comment

  1. ufa

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-za-kutunza-nywele-wakati-unanyonyesha/ […]

Comments are closed.