Hatudhani kama kuna mwadada wa sasa hivi ambae amekosa wig katika kabati lake, karibu kila mtu anayo mawili au matatu ina tegemea na uhitaji wa mtu na mtu, well wigs ni must have’s maana zina rahisisha vitu vingi kama kutafuta wasusi wa haraka ikiwa umepata mtoko wa haraka. Kitu kigumu katika wig ni jinsi ya kulijali lisiharibike iwe ni human hair au synthetic wig.
Leo tunakuletea njia chache za kufanya ili kutunza wig lako
Human hair wig yanakubali moto una weza ku tone au ku pass wakati synthetic ni yale ya plastic ukipass yana yeyuka, unacho takiwa kujua ni tofauti kati ya haya ma wig mawili kama huna uhakika itabidi usome maelezo katika wig lako, hii itakusaidia kuto kuunguza wig lako.
- Wekeza Katika Shampoo Na Conditioner
Kama ulikua ujui basi acha tukujuze kuna shampoo na conditioner ambazo zenyewe zimetengenezwa kwa ajili ya mawig tu, na hii ni kwa sababu ya tofauti ya nywele za asili na bandia, kemikali zilizopo kwenye shampoo au conditioner ya nywele za asili ni kali kulinganisha na kemikali zilizopo katika shampoo na conditoner za ma wig
Kutumia shampoo ya kawaida kwenye wig yako inaweza kuharibu texture ya nywele au kuifuja na kufanya wig lako lijikunje, hivyo uwe makini kuwekeza katika bidhaa hizi. Mbinu yako ya kuosha inapaswa kuwa tofauti, pia – weka wig yako katika shampoo na maji na paka conditioner kisha chana taratiibu wig lake. Suuza na maji ya moto, kisha iache ikauke. wekeza kwenye brashi ya wig ili kuchana na kuondoa mikunjo ya nywele
- Usitumie dawa ya kung’aza nywele au spray katika wig yako
Wengine wanasema kunyunyizia spray wig lako ni sawa, na watu wengi hufanya hivyo bila kuharibu nywele. Hata hivyo, ikiwa unaendelea kunyunyizia wig lako na bidhaa tofauti linaweza kuwa mafuta na kuharibu wig ukashindwa kulimage na kuweza kulitumia tena . Inashauriwa kuepuka kunyunyizia wig lako na aina yoyote ya spray.
- Usitumie moto ku-style au kukausha wig lako
Kama ilivyo katika nywele zako mwenyewe, kutumia moto katika nywele kunaweza kuharibu nywele. Ikiwa una wig la synthetic, joto kutoka kwenye chuma cha curling au hair dryer linaweza kusababisha wig kuyeyuka. Ikiwa hujui jinsi ya kutengeneza wig lako, nenda salon wa kusaidie kufanya mabadiliko unayotaka. Kidokezo
- Usilale au kuoga kwa wig lako
Kuosha wig lako ni lazima, lakini zaidi ya hayo, unatakiwa kuhepuka maji iwezekanavyo. Ondoa / vua wig lako wakati upo katika bwawa, unaoga au mvua nzito. Unapaswa kuepuka kulala ukiwa umevaa wig lako ili kuepuka kujikunja wakati unageuka geuka usingizini.
Ni matumaini yetu hizi tips zitakusaidia.
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-za-kutunza-wig-lako/ […]
… [Trackback]
[…] There you can find 82955 more Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-za-kutunza-wig-lako/ […]
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-za-kutunza-wig-lako/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-za-kutunza-wig-lako/ […]
… [Trackback]
[…] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/njia-za-kutunza-wig-lako/ […]