SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Ondoa Chunusi Za Mgongo Kwa Kutumia Sukari Na Mafuta Ya Nazi
Skin Care

Ondoa Chunusi Za Mgongo Kwa Kutumia Sukari Na Mafuta Ya Nazi 

MGONGO  ni moja ya kiungo cha mwili ambacho kinahitaji uangalizi mzuri.Bila hivyo huleta tabu hasa pale mgongo unapokuwa hauko katika muonekano mzuri. Uchafu unaoganda kwenye mgongo hupelekea muwasho wa mara kwa mara na mgongo kuwa na mabaka mabaka.
Ukweli ni kuwa jaribu kuangalia mgongo wako na kuona kama unastahili kuwa hivyo na kama haustahili basi chukua hatua kwa kuhakikisha mgongo unakuwa safi na kutafuta tiba ya chunusi au mabakamabaka yaliyo mgongoni mwako.


Unapoufanyia tiba mgongo kwa kutumia sabuni za dawa au lotion utaufanya uwe na muonekano mzuri na hata kuwa huru kuvaa nguo yoyote. Wengi wanashindwa kuvaa nguo za wazi kutokana na muonekano wa ngozi zao za mgongoni kuwa mbaya zenye vipele, chunusi na kupauka.
Madoa kwenye mgongo yamekuwa yakikosesha wengi raha kutokana na suala la utunzaji mgongo halitiliwi maanani kama ilivyo kwenye utunzaji wa uso au miguu.


Tumia brashi laini lenye sababu ya kutosha katika kusugua mgongo wako. Kisha paka mafuta.


Kama huwezi kufikia vizuri mgongo kwa kutumia brashi basi unaweza kuomba msaada ili mradi mgongo  utakate na kuwa katika sura ya kupendeza. Wengi wanashindwa kuvaa nguo za wazi kutokana na migongo yao kuwa na sura isiyopendeza.


Ni muhimu ukazingatia usafi wa mgongo ili uwe huru kuvaa nguo za wazi bila kuwa na mashaka kuwa kuna watu wanautazama vibaya mgongo wako na wengine wameanza kucheka.


Aina za Chunusi za mgongoni hazitofautiani  sana na zile za usoni kabisaa. 
Vifuatavyo ni vile ambavyo unaweza kuandaa nyumbani kwako kutoa chunusi za mgongoni. 


1. Scrub ya sukari. 

Mahitaji Nusu kikombe cha sukari Nusu kikombe cha Mafuta ya lozi au zaituni ama Mafuta ya Nazi. 


Chukua sukari yako nusu changanya na Mafuta vizuri. 
Tumia mchanganyiko huu Kama scrub yako kutoa uchafu na taka taka zote kwenye mgongo wako ukiwa unaoga. 
Baada ya kuoga, kausha kwa nguo kavu Kisha paka mafuta ya Nazi kidogo Kama kilainishi! 


Ufanye Mara ngapi? Ufanye kwa wiki mara mbili. 
Kwa nini hii inafanya kazi. Sukari inaweza kukupa mgongo mzuri usio na Chunusi kabisa. 


Kufanya scrub kutakusaidia kuondoa ngozi yote iliyokufa ambayo inasababisha hizo Chunusi mgongoni.


Jee unasafishaje mgongo wako? 

Imeandikwa na @binturembo

Related posts

1 Comment

  1. Darknet market links list 2023

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/ondoa-chunusi-za-mgongo-kwa-kutumia-sukari-na-mafuta-ya-nazi/ […]

Comments are closed.