SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Ondoa Harufu Mbaya Kinywani Kwa Kutumia Mdalisini, Limao Na Asali
Lemon, honey and cinnamon sticks on turquoise blue background with copy space. Top view or flat lay.
Dondoo

Ondoa Harufu Mbaya Kinywani Kwa Kutumia Mdalisini, Limao Na Asali 

Muonekano wako mzuri utakamilishwa na Jinsi utakavyotabasamu, na vile utakavyoweza Kuongea kwa kujiamini. Tabasamu zuri na mwanana linakamilika pale unapokuwa na ngozi yenye afya njema na kinywa chenye harufu nzuri na meno yenye kung’aa.
Leo baada ya kusoma Makala hii, Utaweza kujisaidia kuondoa harufu mbaya kinywani.
Harufu mbaya ya kinywani  inasababishwa na bakteria. Huu ni ugonjwa unaofahamika kitaalamu kama halitosis. Ugonjwa huu unatokana na tabia isiyofaa ya kutotunza kinywa. Na endapo mdomo wako unatoa harufu mbaya sana basi ni dalili za tatizo kubwa zaidi. Onana na Daktari wako mapema
Kutoa harufu mbaya mdomoni kunaweza kuwa kubaya zaidi kutokana na aina ya vyakula unavyokula na mwenendo mbovu wa lishe.
 • KILE UNACHOKULA KINAATHIRI HARUFU YA MDOMO
Kimsingi vyakula unavyokula hupondwapondwa kwa kuanzia mdomoni. Endapo unakula vyakula vyenye harufu kali, kama vile vitunguu maji na vitunguu saumu, harufu kali itabaki kinywani. Kupiga mswaki au kusukutua kwa dawa ya maji ya meno hakutaonda harufu hiyo. Harufu haitaondoka mpaka baada ya muda mrefu kidogo.
Vipande vya vyakula ulivyotafuna hujishikiza katikati ya meno na kwenye fizi. Hivi ndivyo hushambuliwa na bakteria na kusababisha kutoa harufu endapo hautakuwa na tabia ya kusafisha kinywa chako  au kusukutua mdomo kila baada ya mlo.
 • UNAKABILIANAJE NA TATIZO LA KUTOA HARUFU MBAYA KINYWANI ?
Wengine hutumia vitu tofauti tofauti, vyote vikiwa na lengo la kuondoa Harufu mbaya kinywani!  Unaweza kuondoa harufu mbaya  kwa kutumia mchanganyiko wa asili, Mdalasini na Limau
 • JEE WAJUA ASALI, MDALASINI NA LIMAO INAWEZA KUKUONDOLEA HARUFU MBAYA KINYWANI!?

Vitu vitatu vikuu kukusaidia kuanza kunukia:

Asali halisi na mbichi ina sifa za kukabiliana na bakteria. Asali itaua bakteria wabaya wote ndani ya mdomo, tofauti na sukari ambayo huchochea kuzaliana kwa bakteria hao mdomoni.

Mdalasini huua bakeria wasababishao harufu mbaya. Kimsingi tunashauriwa kuwa na mazoea ya kutafuna mdalasini kila siku.

Na kwa hakika Muungano wa Kimataifa wa Utafiti wa Tiba ya Kinywa (International Association for Dental Research) uligundua kuwa watu waliotafuna mdalasini walibainika kupunguza maambukizi ya bakeria wabaya wa kinywa kwa asilimia 50%

Limao ina sifa ya kung’arisha meno. Ina ladha ya kupendeza, inayoburudisha, na husafisha kinywa kwa kuwaondoa bakteria waliojificha ndani kabisa ya fizi na meno.

Zingatia tu kwamba unapoandaa dawa ya kinywa usiweke limao nyingi kwa sababu inaweza kuharibu meno.
Mahitaji
• Juisi iliyotokana na limao 2 zilizovunwa hivi karibuni.
• Nusu kijiko (1/2) ya unga wa mdalasini.
• Nusu kijiko cha baking soda (sodium bicarbonate)
• Kijiko 1 cha asali
• Kikombe kimoja cha maji moto kiasi
• Chupa safi au kikombe safi
MAELEKEZO
1. Changanya vyote hivi kwenye chupa safi au kikombe tupu kisha tikisha moaka vichanganyike sawia.
2. Baada ya kupiga mswaki sukutua kwa dakika chache mchanganyiko huu.
3. Usisukutue mchanganyiko huu zaidi ya mara moja kwa siku. Tumia asubuhi zaidi.
Furahia harufu nzuri na murua baada ya siku chache. Utaona mabadiliko. Jee ulikuwa unafahamu kuhusu hili!? Shea na uwapendao.
Imeandaliwa na kuandikwa na @binturembo

Related posts

6 Comments

 1. Visit Website

  … [Trackback]

  […] Read More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/ondoa-harufu-mbaya-kinywani-kwa-kutumia-mdalisini-limao-na-asali/ […]

 2. xenical weight loss pill​

  … [Trackback]

  […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/ondoa-harufu-mbaya-kinywani-kwa-kutumia-mdalisini-limao-na-asali/ […]

 3. Achieving financial freedom

  … [Trackback]

  […] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/ondoa-harufu-mbaya-kinywani-kwa-kutumia-mdalisini-limao-na-asali/ […]

 4. ปั่นสล็อต

  … [Trackback]

  […] Read More on that Topic: afroswagga.com/urembo/ondoa-harufu-mbaya-kinywani-kwa-kutumia-mdalisini-limao-na-asali/ […]

 5. 다시보기

  … [Trackback]

  […] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/ondoa-harufu-mbaya-kinywani-kwa-kutumia-mdalisini-limao-na-asali/ […]

 6. diamond fire https://exotichousedispensary.com/product/diamond-fire/

  … [Trackback]

  […] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/ondoa-harufu-mbaya-kinywani-kwa-kutumia-mdalisini-limao-na-asali/ […]

Comments are closed.