Utashangaa sana kwamba asali ndiyo hasa kitu kitamu ambacho kwa miaka mingi watu wamekuwa wakikifananisha na raha.Hii inatokana na ukweli kwamba asali inachukua nafasi ya pekee katika dunia ya mwanadamu.Nafasi hii ya pekee imo katika mambo mengi mpaka mwenye tiba kwa kawaida asali ni dawa ya kukabiliana na vitu vingi pamoja na vimelea. Pamoja na kuwa na antiseptic pia ina moisturizer na pia ina antioxidants na inasaidia kukabiliana na uzee.
Uwepo wa kiwango kikubwa cha sukari katika asali kunaipatia uwezo wa dawa na ndiyo maana kwa miaka maelfu imesaidia watu kutibu vidonda.
Mtaalam mmoja wa ngozi mwenye makazi yake mjini New York City ambaye pia ni daktari, Amy Wechsler anasema hali ya kunyunyurika iliyonayo asali na inayonasa inafanya kuwa kinga imara katika kidonda ambacho kinahitaji kisiingiliwe na vimelea na kutoa mazingira ya kuponya, hivyo asali ni bomba kwa tiba.

Pamoja na tiba asali ni moisturizer babu kubwa kwa ajili ya Ngozi ya mwili pia. Asali ni dawa ya asili ambayo ina uwezo wa kukusanya maji kutoka ndani ya misuli hadi katika sehemu za juu za ngozi na hivyo kusaidia kuondoa mikunjo.
Mimi nakushauri jaribu moisturizing ya asali ambayo itaondoa ukavu wa ngozi yako na hata kuwasha na kutatarika.
- Changanya vijiko vya mezani viwili vya asali na vijiko viwili vya mezani vya maziwa.
- pasha moto mchanganyiko huo
- kisha paka mchanganyiko huo katika mwili wako na kupumzika kwa dakika kama kumi hivi.
- Kisha jioshe kwa maji ya vuguvugu.Kama unataka kitu kama kosmetiki agiza lotion ya asali ili kuweka sawa ngozi yako.
Hakikisha unanunua lotion ambayo imetengenezwa kwa asali isiyochujwa.
Aina zote za asali zinasaidia kuondoa mikunjo ya uzeeni.
Tahadhari : Usifanye hii usoni! Itaongeza mafuta na utakuwa kwenye hatari ya kupata chunusi.
Related posts
HOT TOPICS
Happiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/VZ1jH2zJUg
FollowHappiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/689j7Yjcn0
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
Feza Kessy Atuelezea Kuhusu Fashion & Style Zake
Feza Tadei Kessy ni Muimbaji, Muigizaji lakini pia ni mtunzi wa nyimbo lakini pia Fezza ni former beauty queen ambapo mwaka 2005 alikuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala & Miss Tanzania Runner up. Lakini pia alishawahi kuwepo katika Reality Tv Show – Big Brother Africa. Kwa…