SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

One On One With Makeup Artist Queen Nuru
Make Up

One On One With Makeup Artist Queen Nuru 

Kama tutatakiwa kutaja makeup artist bora Tanzania basi Nuru nae atakuepo kwenye list yetu, ukiachana na kazi yake nzuri lakini pia she is so humble na ana customer care nzuri, tumemjua Nuru kupitia Instagram ambapo anajiita Queennuru_makeup akiwa bado hajafikisha 55k followers ambao anao sasa. Nuru ni professional makeup artist ambae amesomea maswala ya makeup kutokana na kazi yake nzuri amesha fanya kazi na baadhi ya watu maarufu kama Nandy, Zari, Hamisa, Ruby na wengine wengi na haya ni mawili matatu tuliyo yatoa kutoka kwake.

Afroswagga – Ulianza Vipi Mpaka Kufikia Hapa?

Nuru – Baada ya kumaliza masomo yangu ya sekondari,sikuendelea na elimu ya juu,hivyo nikaajiriwa katika kampuni ya SHEARILLUSION hapo ndipo safari yangu ilipoaanza.

Afroswagga – Nini Kiliku Inspire Kufanya Makeup?

Nuru – Nilifanya kazi kwa muda wa miaka 3 na wakati niko katika kampuni hiyo  nilichaguliwa kushiriki katika program iitwayo MANJANO DREAMMAKERS ambayo ilinipa elimu ya upambaji(makeup artistry),hivyo safari yangu ya kuanza kupamba ilianza mwaka 2015 mpaka kufikia sasa.
kilichonifanya nifanye kazi hii nni kwasababu nilipenda sana kuona watu wanapendeza kupitia mikono yangu na pia bosi wangu aliona kipaji changu ndio mana alinichagua kushiriki katika kupata elimu ya upambaji.

Celeb Wako wa Kwanza Kufanya Nae Kazi Alikua Ni Nani Na Ilikuaje?

Afroswagga – Celebrity wa kwanza kufanya nae makeup alikuwa Rose Ndauka..,na yeye alipata habari kutoka kwa marafiki zake ambao tayari niliwahi kuwapamba kwahiyo akanipigia simu kuwa nahitaji kufanyiwa makeup ndipo tulipokutana na nikampamba.

 


Afroswagga – Je Unatumia Local Brands Za Tanzania? Kama Manjano, Eye Lashes Za Watanzania Na Lipsticks? Ubora Wake Upoje

Nuru – Natumia local brands za makeup kama vile LUVTOUCH MANJANO, pia natumia lashes za Lavie na lipstick za Luvtouch pia,na ubora wake ni mzuri sana na hata wateja wangu wanafurahia sana.

Afroswagga – Tofauti ya makeup ya Celeb akiwa anaenda jukwaani na kwenye events kubwa ni IPI?

Nuru – Makeup ya celeb akiwa anaenda kwenye event huwa ni ya kawaida tu yanI simple evening makeup kwa kuwa haiitaji awe na vitu vingi usoni ila akiwa anapanda jukwaani au kwenye show inakuwa kidogo creative kwakuwa atapigwa picha na details za makeup zinapaswa kuonekana vizuri zaidi kwahiyo huwa tunamfanyia contour na pia hata rangi za eyeshadow zinabidi ziwe kidogo zinaonekana.

Afroswagga – umesha wahi kunfanyia MTU makeup na ukakosolewa mitandaoni?  Kama yes ulipokeaje ?

Nuru – Nimewahi kufanya makeup na kwenye mitandao nikakosolewa mfano nilipomfanyia simple makeup ZARI ila nilipokea kama changamoto kwenye kazi ambayo imenisaidia kuwa makini zaidi na kufanya kazi nzuri zaidi japo unapopokea kasoro lazima woga uwepo kwa hali ya kibinadamu.

Afroswagga – Umeshawahi Kufanya Makeup Za Fashion Show?

Nuru – Nimewahi kufanya makeup kwa ajili ya fashion show mwaka 2015

Afroswagga – Ni kweli huwa mnawapa watu was kawaida wanafunzi wawahudumie huku nyie mkichagua tu celebs?

Nuru – Si kweli kuwa tunawapa wanafunzi wapambe watu ambao si maarufu kwetu mteja yoyote ni mwenye thamani sana na kwenye saloon yetu wote ambao wanapamba si wanafunzi kwakuwa
kwakuwa tayari wamepitia mafunzo ya upambaji na tunamshukuru Mungu hatujawahi kupata malalamiko kwakuwa wote wanafurahia makeup wanapotoka ila ile tu hulka ya watu kutaka kupambwa na mtu waliyemzoea ipo ila tukiwaelewesha huwa wanakubali kupambwa na mtu yeyote ambaye ni mpambaji saloon kwetu.


Afroswagga – nani unependa kufanya nae kazi mbeleni?
Nuru – Ningependa kufanya kazi hii ya upambaji na celeb kama hawa hapo baadae  mfano Wema Sepetu  na Elizabeth Michael hawa ni celeb ambao natamani kuwapamba siku moja Mwenyezi Mungu akijaalia


Afroswagga – waambie wa Tanzania kwanini wamchague nuru na sio makeup artist wengine

Nuru – Nawaomba watanzania wanichague mimi kuwafanyia makeup kwasababu;
1.Ninao ujuzi wa kufanya makeup na mpaka sasa nina uzoefu wa miaka 3

2.watakapofanyiwa makaeup watafurahia na hawatajutia kwakuwa kila mtu atabaki na rangi yake kwakuwa mimi ninachofanya si kubadili rangi ya mtu kutoka uhalisia wake ila ni kumpend
kumpendezesha na kumwongezea thamani katika urembo wake

3.Bei zangu ni nafuu kabisa ambazo mtu yoyote anaweza kulipia

Nuru anapatikana sinza africasana  ana fanya makeup za aina mbalimbali kamaSend off,Harusi,Kitchen party,Video Shooting,graduation unaweza kumpata hapa pia  ☎ 0656442475)

Related posts

5 Comments

 1. sig spear msrp

  … [Trackback]

  […] There you can find 16779 more Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/one-on-one-with-makeup-artist-queen-nuru/ […]

 2. hidden cam couple bbw in the beach sex

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/one-on-one-with-makeup-artist-queen-nuru/ […]

 3. 티비위키

  … [Trackback]

  […] Read More here on that Topic: afroswagga.com/urembo/one-on-one-with-makeup-artist-queen-nuru/ […]

 4. Tropicana cherry https://exotichousedispensary.com/product/tropicana-cherry/

  … [Trackback]

  […] Here you can find 63012 additional Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/one-on-one-with-makeup-artist-queen-nuru/ […]

 5. SIMPLEPLAY COMPANY มีความเป็นมาอย่างไร?

  … [Trackback]

  […] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/one-on-one-with-makeup-artist-queen-nuru/ […]

Leave a Reply