Kutumbua chunusi na vipele ni tabia ya wengi ambayo husababisha makovu, wekundu na kusambaza bacteria (hupelekea matatizo zaidi ya ngozi) kwenye maeneo ya ngozi ambayo hayana matatizo.
Japokuwa ni ngumu kutotumbua mchunusi unaokutazama, Fanya yafuatayo kila unapofikiria kutumbua chunusi
- Kutumbua chunusi kunaacha makovu.Kama ulikuwa hujui ndio ujue kuanzia leo, kwamba chunusi inayotumbuliwa inaacha kovu na madoa meusi ambayo huchukua muda kuondoka kulikoni ile isiyotumbuliwa, kovu au doa lake huchukua muda mfupi sana kuondoka.
- .Ukitumbua chunusi unachelewesha uponyaji “healing process” na kwa sababu hiyo ngozi yako huchelewa kupona na kubaki na makovu
- Unasambaza bacteria na ndio maana ukitumbua chunusi moja leo kesho unapata nyengine unatumbua tena na unabaki na makovu na chunusi zisizoisha! Usitumbue chunusi

Njia ya kuacha kutumbua chunusi
- Usipende kushika kushika uso wako.Ukiwa unajishika shika utapata hamasa ya kujitumbua chunusi.
- Acha kujiangalia kwenye kioo na kuona wewe pekee ndie uliebarikiwa chunusi nyingi zaidi! Ukweli ni kwamba wala hakuna anaekuangalia kama unavyojiangalia wewe. Wewe utaona una machunusi mengi na wala hakuna anaeshughulika nazo. Jifunze ku relax.
- Kama ni lazima na hutaki kuona hizo chunusi zilizojitokeza tumia SOS spot gel hii inaondoa chunusi unayotaka kuitumbua na wala haiachi makovu. Unarudia kupaka kila baada ya masaa 8.
©️binturembo
Related posts
3 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/pata-kufahamu-madhara-ya-kutumbua-chunusi-na-namna-ya-kuacha-tabia-hio/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/pata-kufahamu-madhara-ya-kutumbua-chunusi-na-namna-ya-kuacha-tabia-hio/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/pata-kufahamu-madhara-ya-kutumbua-chunusi-na-namna-ya-kuacha-tabia-hio/ […]