So kuna hii meme vile imetrend sana na kwa vile tuko obsessed na skin care tuongelee hiyo imekaaje,meme hio inalinganisha mwanaume ambae anatumia taulo yake kufutia kila kitu na akiweka usoni haina shida ila kwa mwanamke ambae ana stick skin care routine yake bado chunusi zinagoma.

Kwanza ni hali ya kawaida na hiyo inachangiwa na sababu zifuatazo:
- Vichocheo mwilini ndio vya kulaumiwa.
Wanawake wanapata mabadiliko ya homoni wakati wa hedhi, wakati wa ujauzito, na wakiwa wanaelekea kukoma hedhi. Wanawake hupata chunusi zaidi kwa sababu ya mabadiliko ya homoni kuliko Wanaume.-Madaktari hutoa dawa kwa ajili kucontrol homoni kama vidonge vya uzazi wa mpango kwa ajili ya wanawake.
- Nini ujifanyie ukiona mabadiliko:
1. Kwanza jichunguze, ujue unapopata mabadiliko ya homoni kwa mfano ukiwa kwenye hedhi yako jiangalie jee unapata mabadiliko gani? Utulie usianze kutafuta vipodozi vipya, maana mara nyingi hali hiyo haidumu ukimaliza hedhi yako tu na chunusi zimeisha.
2. Pili Kama una ujauzito, ama unaelekea ukomo wa hedhi yako “menopause” uwe na amani kabisa maana chunusi zinaenda na kurudi.
3. Na wale wenye wanabadili vipodozi kila baada ya wiki moja yaani siku 7 unahitaji uvumilivu wakati mwengine ni vile ngozi yako tu inaamua kufanya hivyo.
4. Wanawake wanapata chunusi zaidi kuliko wanaume kwa sababu wao wanapitia mabadiliko ya vichocheo mwilini ambayo hufanya chunusi kuja kwa wingi zaidi.
5. Relax, Cha kwanza ukiona mabadiliko yoyote kwenye ngozi yako jifunze kutulia. Huku unaangalia utaratibu wa nini ufanye sio ukimbilie vipodozi maana na vyenyewe vinachukua muda hadi uone matokeo, nazungumzia vile salama kwa matumizi ya binadamu kama unataka bandika bandua bado utakuwa hujatatua tatizo lako badala yake utakuwa unazidisha.
©️binturembo
Related posts
4 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/pata-kujua-tofauti-ya-matatizo-ya-ngozi-kati-ya-wanaume-na-wanawake/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/pata-kujua-tofauti-ya-matatizo-ya-ngozi-kati-ya-wanaume-na-wanawake/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/pata-kujua-tofauti-ya-matatizo-ya-ngozi-kati-ya-wanaume-na-wanawake/ […]
… [Trackback]
[…] Find More here on that Topic: afroswagga.com/urembo/pata-kujua-tofauti-ya-matatizo-ya-ngozi-kati-ya-wanaume-na-wanawake/ […]