SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Pata Kujua Zaidi Kuhusu Phyna Lashes
One on One

Pata Kujua Zaidi Kuhusu Phyna Lashes 

Kama mabvyo Mheshimiwa Rais amesema kutaka Tanzania ya Viwanda basi ndivyo ambavyo wa-Tanzania tunafanya kwa sasa, kila mmoja anajaribu kufanya na kugundua kile ambacho ana kipenda na kukifanyia kazi. Kuna na Phina au Phyn, yeye anauza Fake Eye Lashes ambazo anatengeneza mwenyewe yaani ni bidhaa yake, tumekutana na Phyn instagram na tukaona si mbaya kama tutafanya nae interview na kupata mawili matatu kutoka kwake
Afroswagga : Tuambie Kuhusu Background yako mpaka kufikia maamuzi ya kuuza bidhaa zako mwenyewe za nyusi bandia
Phyn : Naitwa Phina Revocatus  ,nilikuwa miss ifm na miss vyuo vikuu mwaka 2012′ pia nilishiriki miss Tanzania mnamo mwaka 2012. kikubwa kilichonifanya niuze bidhaa zangu mwenyewe za nyusi bandia ni kwanza napenda kope na urembo kwa ujumla,pili naamini kwenye kujiajiri na kufanya kazi kwa bidii.
Afroswagga : Tuambie Kuhusu Phyn Lashes
Phyn : Phynlashes ni kope za bandia ambazo zinatengenezwa kutumia asilimia Mia ya nywele za binadamu, ni laini na hazina madhara yoyote kwa macho ya binadamu. Pia unaweza kutumia phynlashes zaidi ya Mara moja , unaweza kutumia zaidi ya siku 30(mwezi) inategemea na utunzaji wako.
Afroswagga:  Kuna kampuni nyingi za false eye lashes je phynlashes zina tofauti ipi na hizi nyingine?
Phyn : Tofauti ya phynlashes na kope nyingine, kope nyingi ni  plastic lakini phynlashes ni asilimia mia nywele, pia kope nyingne hazidumu nyingi ukitumia mara moja huwezi kurudia lakini phynlashes unaweza kutumia  Mara 30 na zaidi inategemea na utunzaji wako.
Afroswagga: Nini kina ku-inspire?
Phyn : Kufanya kazi kwa bidii na kufikia level za brand kubwa kama kylie cosmetics/mac cosmetics/lashed by blacchyna etc.
Afroswagga : Tupe beauty tips 3 ambazo you live by
Phyn : My 3 beauty tips are
1: I always treat my skin right
2:i make sure I do my nails
3: and lastly I make sure my hair and eyelashes  are on fleek
Afroswagga: Mpaka sasa una collection ngapi za eye lashes?
Phyn : Mpka sasa nna collection 2 ,
1:kope za mojamoja ambazo unaweza ukabandika,ukalala nazo ,ukaoga nazo
2: kope za kubandika na kubandua ambazo unaweza ukatumia wakati unatoka na kuzibandua ukirudi ;katika kope hizi za aina ya pili nnastyle tofauti tofauti ambazo kuna
   buff style,
   diva style,
  goddess style ,
inategemea tu mteja atahitaji style gani.
Afroswagga: tuambie kwanini tununue phynlashes na si lashes nyingine?
Phyn : Nawashauri warembo kutumia phynlashes  sababu zinakaa sana kuliko kope nyingne, pili ni nyepesi huwezi kusikia uzito wa jicho baada ya kuweka,pia zinatoa muonekano wa asili ( natural look)sababu zimetengenezwa na nywele na ni ngumu mtu kujua kama umebandika kope bandia wengi hujua ni kope zako zimejaa tu.
Afroswagga: Nini unadhani kifanyike ili ninyi ambao mnaanza kuwa na brand zenu zifike pale mnataka ziwe?
 Phyn : Kikubwa ni hard working, creativity, confidence na support kutoka kwa watanzania
Afroswagga: Je ni vipi wa Tanzania wanaweza kupata bidhaa zako?
Phyn : Phynlashes tupo kwenye mitandao ya jamii kama Facebook,instagram,snapchat  kwa kutumia username :PHYNLASHES ! Pia tunapatikana whatsapp kupitia number 0754946520
Email: phynlashes @ gmail.com
Pia website yetu itakua tayari soon
Afroswagga : ukiachana na hizi eye lashes kuna kingine tujiandae kukipata kutoka kwako?
Phyn : Tukiachana na kope nna bidhaa nyingi ntaleta, siwezi kusema ni bidhaa gani kwa sasa ! Lakini napenda kuwaambia wapenzi wa bidhaa zangu wakae mkao wa kula , I have so many products am still working on and soon they will be out .
Afroswagga: chochote ambacho ungependa kuwaambia wa Tanzania 
Phyn: Napenda kuwashauri watanzania especially vijana kujiajili, there’s so many opportunities outside .. tuondoe mentality ya ukimaliza shule lazima kuajiliwa .
 Pili tusupport brand zetu za ndani nchi.
Kama ungependa kuwa-follow click hapa @phynlashes 

Related posts

4 Comments

  1. the original source

    … [Trackback]

    […] There you will find 46908 more Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/pata-kujua-zaidi-kuhusu-phyna-lashes/ […]

  2. passive income ideas

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/pata-kujua-zaidi-kuhusu-phyna-lashes/ […]

  3. go to the website

    … [Trackback]

    […] Here you can find 19570 additional Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/pata-kujua-zaidi-kuhusu-phyna-lashes/ […]

  4. cablagem informática

    … [Trackback]

    […] There you can find 80495 additional Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/pata-kujua-zaidi-kuhusu-phyna-lashes/ […]

Comments are closed.