Aliesema “Mwanamke Urembo” hakukosea, wanawake wengi upenda urembo, wanapenda kila kitu chao kionekane kizuri na smart. Na leo tunakuletea namna ambavyo unaweza kusafisha miguu yako ipate muonekano mzuri kwa kutumia chumvi,asali na maji ya uvuguvugu hii njia ni kwa wote wanaume kwa wanawake.

Zifuatazo ni njia za kuosha miguu

Chukua mchanganyiko wa maji ya uvuguvugu na  chumvi,
unapoanza kusafisha unyayo wako weka miguu katika maji ya moto kiasi, kwa muda wa dakika 5 kisha anza kusafisha kwakusugua hakikisha mabaki ya ngozi yanaisha katika miguu yako
Weka mchanganyiko wa maji pamoja na asali,
ambayo husaidia kulainisha ngozi ya Unyayo wako pamoja na kuondoa michubuko iliyopo katika Unyayo.
Futa miguu yako kwa kitambaa safi 
kuanzia katika vidole vyako. Usipo kausha vema hupelekea kupata fangasi na kupelekea miguu kunuka unapokuwa umevaa viatu vya kudumbukiza.Watu walio chanika miguu wanashauriwa kutumia viatu vya kudumbukiza kwa muda mrefu huku ukizingatia taaratibu za usafishaji wa nyayo, pia unaweza kutumia cream za kulainisha Unyayo wako ambazo hupatikana katika maduka ya vipodozi, zinajulikana Kama Foot Cream
Pendelea kutumia mafuta ya watoto kujipaka katika Unyayo wako(baby Oil) 
au paka Grisalini(glyceline) kwenye unyayo kisha vaa soksi wakati wa kulala, Soksi husadia kulainisha Unyayo wako kutokana na hali ya joto  inayokuwepo ndani ya soksi.
Ongeza kiwango cha kunywa maji,
kila siku jitahidi kunywa angalau lita tatu ya maji  ambayo husadia  ngozi yako kuendelea kuwa  nyororo.
Imeandaliwa na kuandikwa na @binturembo