Wengi huwa tunasema kufanya mazoezi ni kazi na tunaweka ugumu na visingizio kadha wa kadha kama muda wa kufanya mazoezi hatuna na mengine mengi, lakini tunapenda sana kuwa na tumbo dogo na kupata lile umbo namba 8 alilo liimba Daz Baba kipindi hicho. Lakini si lazima kufanya mazoezi kuna njia mbali mbali za kupunguza tumbo endapo tu utakuwa serious kufanya. Leo tunakuleta njia moja wapo ya kupunguza mafuta ya tumbo ambapo ni kunywa maji ya tangawizi

Faida za tangawizi katika kupunguza mafuta ya tumbo

  • Tangawizi inasaidia punguza  mafuta na  kuboresha mmeng’enyo wa chakula
  • Tangawizi husaidia kupambana na seli za mafuta katika mwili hasa katika eneo la tumbo.
  • Tangawizi pia huzuia uhifadhi wa maji unaozuia au kusababisha bloating

Mahitaji 

  • Tangawizi 1Inch – Moja
  • Maji – kikombe kimoja

Namna ya kutengeneza maji ya tangawizi

  • osha na menya tangawizi yako
  • kisha katakata vipande vipande vya size na uchanganye na maji yako ya moto
  • acha vipande vya tangawizi vikae katika maji hayo kwa dakika 5-10 kisha viondoe vipande vya tangawizi kabla hujanywa.
  • Unaweza kuongezea asali ukipenda.
  • unaweza kunywa maji haya muda wowote katika siku.