Kama kuna kitu ambacho ni sawa na ndoto mbaya basi ni kucha kukatika, hasa kwa wafugaji na wapenda kucha zao. Kucha ikikatika maana yake ni moja ukate zote au uwe na kucha moja fupi nyingine ndefu ambapo mara nyingi huwa haivutii, lakini kumbe unaweza kutumia karatasi la jani la chai kurekebisha kucha hio na mtu asijue kama kuna moja ime katika.

MAHITAJI.

 • Karatasi la jani la chai
 • rangi ya kucha nyeupe ya chini (base coat)
 • rangi ya kucha chaguo lako
 • mkasi
 • rangiya kucha nyeupe ya juu (top coat)

NAMNA YA KUFANYA.

 • Kama ulipaka rangi ifute
 • chukua jani la chai toa majani ya chai, chukua karatasi la jani la chai kata pembe nne iwe nusu ya kucha yako urefu uutakao au uwe sawa na zile kucha nyingine.

Tea_bags

 • paka rangi yako ya kucha nyeupe ya chini (base coat) kisha weka kile kipande cha karatasi la jani la chai ulilo likata na hakikisha imekaa vizuri kabisa bila kuacha hewa.
 • baada ya hapo paka tena base coat yako juu ya karatasi la jani ya chai, iki kauka paka tena

tea-bag-nail-repair-1

 • Rekebisha urefu na shepu ifanane na kucha nyingine

tea-bag-nail-repair-2

 • paka rangi uitakayo ikikauka paka top coat

MATOKEO YAKE NI HAYA UWEZI ONA TOFAUTI KATIKA HIZO KUCHA!!!

tea-bag-nail-repair-4