SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

ROSE WATER NA MATUMIZI YAKE
Urembo

ROSE WATER NA MATUMIZI YAKE 

Rose Water ni maji yanayo tokana na kuloweka majani ya maua rose katika maji, kinacho patikana hapo hutumiwa kutengeneza Perfume, kuweka kwenye chakula na hata kutumiwa katika urembo. Leo tutaongelea zaidi kwenye urembo

hutumika kama Toner

Acne-remedies-with-rose-water

Rose water inaweza kutumika kutone ngozi yako maana insaidia kupunguza bakteria katika ngozi yako hivyo pia husaidia kuondoa chunusi, inasaidia kuondoa muonekano wa ngozi kuwa na alergy mfano wekundu wa ngozi kwa watu weupe n.k wakati huo huo huipa ngozi yako unyevu na kuituliza ngozi yako. Ukimaliza kusafisha uso wako chukua pamba kidogo iweke rose water na kisha jifute/ paka usoni iwapo una wekundu unaotokana na inflamation(alergy/muitikio wa ngozi) utaona unapotea.
Tunapoongelea toning ni kama hivi, yaani ngozi yako inaenda inalingana na kupata mng’ao

Make Up remover ( Kuondoa Make up)

how-to-remove-makeup
Rose water inasafisha ngozi vizuri unapojifuta na pamba hivyo hata uwe umepaka make up ya kugandia huwa inaondoshwa na rosewater unapofuta. Haya maji huweza kuondoa hata make up zinazoandikwa water proof kama mascara au eye shadow na kuiacha ngozi yako ikiwa na unyevu.

Kutibu nywele

kama una nywele kavu na nyepesi, tumia rose water kuzitibu unacho takiwa kufanya ni baada ya kuosha nywele zako mimina au paka mafuta ya rose water itasaidia kuku conditon nywele zako na kuzing’aza pia una weza kuweka mafuta ya rose water katika shampoo yako ukioshea nywele harufu yake hudumu kwa muda katika nywele na kufanya nywele zako zinukie.

Katika kufanya macho yako yaonekane vizuri
Rose water inasidia kupunguza dark cycles na ile hali ya jicho kuvimba (baggy Eyes) kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa kulala usingizi vizuri. ukichukua pamba yako iliyochovya kwenye rose water itumie kufuta taratibu au kukanda kwa mbali kuzunguka jicho lako baada ya muda jicho linakuwa powa.

Unaweza Kuiongezea katika treatment ya uso
Iwapo wewe ni muumini wa natural treatment kama ya kupaka manjano usoni basi badala ya kuchanganyia maji unaweza kuchanganya na rose water kisha unapaka usoni, hutibu makovu pia na chunusi.

turmeric

 

Related posts

3 Comments

  1. Our site

    … [Trackback]

    […] Read More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/rose-water-na-matumizi-yake/ […]

  2. youtube video downloader free download

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/rose-water-na-matumizi-yake/ […]

  3. Buy Changa DMT online Brisbane

    … [Trackback]

    […] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/rose-water-na-matumizi-yake/ […]

Leave a Reply