Umeshawahi kujiuliza kwanini kipodozi chako hakifanyi kazi ipasavyo? Na unatamani kuachana nacho na kutafuta kipodozi kingine? Well DON’T kuna sababu nyingi sana aambazo huchangia kipodozi kisifanye kazi yake vizuri. Leo tutaongelea sababu hizo.
- Kutokutumia Kipodozi Ambacho Kina-regimen za aina ya ngozi yako
Hapa ndipo unakuja umuhimu wa kujua aina ya ngozi yako na nini kinafaa kutumia, mfano una ngozi kavu ukitumia vipodozi ambavyo ni vikavu basi itazidisha kufanya ngozi yako kuendelea kuwa kavu na kuharibika zaidi.
Jinsi Ya Kujua Aina Ya Ngozi Yako
- Kukata Tamaa Mapema
Kumbuka vipodozi huchukua muda kutoa matokeo, hapa watu wengi huwa tunashindwa kuvumilia tunaruka kutoka kipodozi kimoja kwenda kingine kwa muda wakati mfupi matokeo yake tunaharibu kabisa ngozi zetu kwa mujibu wa expertise wanasema kuona matokeo ya kipodozi huchukua week kadhaa kulingana na regimen zilizopo katika kipodozi na wakati mwingine huchukua hadi miezi mitatu kupata matokeo.
- Kutumia kiasi kisicho sahihi
Hakikisha Unafuata maagizo ambayo huandikwa nyuma ya lebo ya kipodozi ili kuweza kujua ni kiasi gani cha kutumia. Ikiwa bado huna hakika, wasiliana na daktari / mtaalam wako wa ngozi au mtaalam wako wa ngozi. Kutumia kiasi kisicho faa cha kipodozi chako kunaweza kuathiri matokeo.

- Stressful lifestyle
Moja ya sababu kubwa ya chunusi au kuharibika kwa ngozi ni stress, hakuna kipodozi ambacho kitaweza kufanya kazi vizuri endapo hutoweza ku-manage stress. Vitu kama yoga, mazoezi, na facials vinaweza kukusaidia kupumzika wakati unashughulika na stress. Pia hakikisha kupata angalau masaa 7-8 ya kupumzika.
- Kutotumia moisturizer
Unapaswa kutumia kila siku moisturizer baada ya kipodozi chako, ngozi yako italindwa pia endapo utatumia moisturizer.
- Kutokutumia Sunscreen
Sunscreen ni muhimu katika kukinga ngozi yako na miale ya jua, wengi wetu tukipaka tu kipodozi tunahisi tumemaliza na kitafanya kila kitu.
Umuhimu Wa Kupaka Sunscreen Katika Ngozi
Ni matumaini yetu umepata kujua nini ufanye ili kupata matokeo mazuri na kipodozi unachokitumia.
Related posts
HOT TOPICS
Happiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/VZ1jH2zJUg
FollowHappiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/689j7Yjcn0
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
Feza Kessy Atuelezea Kuhusu Fashion & Style Zake
Feza Tadei Kessy ni Muimbaji, Muigizaji lakini pia ni mtunzi wa nyimbo lakini pia Fezza ni former beauty queen ambapo mwaka 2005 alikuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala & Miss Tanzania Runner up. Lakini pia alishawahi kuwepo katika Reality Tv Show – Big Brother Africa. Kwa…