SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Sababu Za Michirizi Mwilini Na Namna Ya Kuondoa
Urembo

Sababu Za Michirizi Mwilini Na Namna Ya Kuondoa 

Michirizi katika ngozi imekuwa kero kwa watu wengi,huku wengi wakihangaika bila mafanikio ya kuondoa tatizo hili,leo tuangalie sababu za kupata michirizi katika ngozi na tiba yake.
SABABU ZA KUPATA MICHIRIZI
  • Matumizi ya kemikali za kujichubua  na vipodozi vikali.
Kemikali za kujichubua huharibu ngozi na kuilazimisha kutengeneza Ngozi Mpya kila Wakati Lakini kwa kufanya hivyo ngozi hutanuka na Ndio michirizi hutokea.
Utakuwa shahidi kama umeaonana na Mwanamke mwenye ametumia vipodozi vikali huwa na muonekano wa ajabu na Michirizi imesalia kwenye Ngozi yake. Vipodozi haramu, vyenye kemikali na viambata sumu havijawa salama Kwa matumizi Kutokana na madhara makubwa ikiwemo Michirizi.
  • Mimba na kujifungua kwa kina mama.

Mabadiliko yanayotekea mwilini Wakati wa ujauzito ni kitu cha kawaida Kabisa. Kama wewe ni mjamzito na umepata Michirizi Unatakiwa kuwa na amani na kuchukua hatua nitakazoeleza Hapa chini.
  • Sababu nyenginezo ni pamoja na kupungua uzito, kunenepa.
Kuongeza mwili kunasababisha ngozi hutanuka na Michirizi inatokea Wakati kupungua kunakuacha na Michirizi iliyoletwa na unene. Sio wanene wote wakipungua hufanya Michirizi ila wengi wao. Na wengine hufanya Jitihada za kuondoa tatizo hilo Wakati wakifanya Jitihada za kupungua.
  • Vile vile ukuaji wa haraka wakati wa kubaleghe, Mabadiliko ya mwili pamoja na Lishe mbovu
Kwa kawaida michirizi hii huwa haimletei mtu maumivu ya aina yoyote,( wengine hupata  Maumivu, onana na daktari wako mapema)  mbali jambo kubwa huwa ni kuubadili muonekano wa ngozi ya mtu. Kwa baadhi ya watu michirizi hii huwa ni mikubwa sana, na kwa namna moja au nyingine humnyima mtu uhuru au humfanya mtu asiwe na amani pundi anapokuwa mbele ya watu kwa kutegemeana na michirizi hiyo imetokea sehemu gani ya mwili.
Unaweza kuiondoa michirizi kwa njia ya asili kwa kutumia:
  • Kahawa
Mbegu za kahawa zilizokaangwa kiasi robo kikombe; twanga au saga kahawa liiyo kaangwa.. Unga wake changanya  na mafuta ya Nazi tumia kupaka hadi uone matokeo. Jipake mara mbili hadi tatu kwa siku. Futa na kitambaa. Mchanganyiko huu pia waweza utumia kama ‘facial’; husaidia ngozi kutozeeka au kuwa na mikunjo ya ngozi.
  • Juisi ya limau na tango

Unahitaji limau moja na tango kipande kidogo. Chuja limau kisha changanya na kipande cha tango na uvisage pamoja. Kisha paka mchanganyiko huu kwenye eneo lenye michirizi na ukae nayo dakika 10. Kisha osha.
Hii ni njia nzuri pia kuondoa hata madoa usoni kwa wenye ngozi za mafuta. Unaweza itumia usoni pia.
Fanya hivi kila siku angalau mara mbili kwa matokeo ya haraka.
  • Viazi mviringo

Unapaswa kuvikata vipande vidogo vidogo vya viazi hivyo kisha uvitumie kusugua sehemu yenye michirizi kisha yaache kwa muda usio pungua saa 1.
Baadaye oga kwa kutumia maji ya uvuguvugu. Njia hii ukitumia kwa muda mrefu angalau mara mbili kila siku husaidia sana kuondosha michirizi hiyo.
  • Kula lishe bora,

unywaji wa maji mengi, angalau glasi nane kwa siku, ulaji wa mboga za majani na vyakula vyenye wingi wa vitamini C na E sambamba na madini ya Zinc na Silica ikiwamo karoti, spinachi na maharage mabichi.
Shea na uwapendao!

Related posts

1 Comment

  1. furbaby

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/sababu-za-michirizi-mwilini-na-namna-ya-kuondoa/ […]

Comments are closed.