Watu wengi sasa hivi wameharibika uso vibaya kutokana na hali ya upepo ambao unasababisha ngozi kuwa mbaya na wengi wamejikuta wakibadilisha badilisha mafuta au cream ya kupaka.
Unaweza kujikuta unabadilisha kila aina ya mafuta lakini bado ngozi yako ikawa mbaya tu na usijue la kufanya.
Leo nimekuletea scrub ya maziwa, asali na limao kwa ajili kukupa matokeo chanya ya ngozi yako.
Mahitaji
- Maziwa ya unga
- Asali
- Juisi ya limao
- Mafuta ya mzaituni au mlozi
Jinsi ya kuchanganya
- Changanya kila kitu kwa usawa, kama ni kijiko kimoja cha asali, juisi ya limao na mafuta ya mzaituni au mlozi vyote viwe sawa. Kama umeamua kutumia nusu kikombe, iwe hivyo kwa vyote.
- Baada ya kupata mchanganyiko wote, changanya na maziwa ya unga ukoroge mpaka upate mchanganyiko mmoja. Angalia kama unavutika, kama unavutika kama cream, paka kwenye ngozi yako.
- Kaa kwa muda wa dakika 15 kisha fanyia masaji taratibu, baada ya hapo osha kuondoa scrub yote. Maziwa yanaifanya ngozi yako kuteleza na kuwa nyororo, inaondoa madhara ya jua na kukufanya uonekane mrembo zaidi.
Asali inaifanya ngozi yako kung’aa zaidi kwani ina kitu kinachong’arisha, limao linakusaidia kusafisha ngozi na kuifanya kuwa ya asili zaidi.
Mafuta ya mzaituni au mlozi yana uwezo wa kuondoa ngozi iliyokufa na kuleta ile inayong’ara.
Shea na uwapendao!
Related posts
HOT TOPICS
The Hardest Part Of Being A Nigerian Bride Is To Comeup With A Bride Look That Wont Match With Any Of The Guest’s A… https://t.co/8vfNPS0IYg
FollowItaly Kumekucha Afromates #TheKardashian #TheKardashian wapo huko kwaajili ya the wedding of the year. Haya mnasubiri lo… https://t.co/kENoAG9RQg
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…