Kwa wapenzi wa urembo wa ngozi basi hili neno si geni masikioni mwako, kwasasa ndio trend kubwa katika ulimwengu wa urembo ambapo watu maarufu na beauty & skincare experts wamekuwa wakiongelea sana kuhusu sheet mask, lakini kama sio mfuatiliaji wa haya mambo inaweza kuwa ndio kwanza unalisikia well tupo hapa kukujulisha kuhusu sheet mask.
- Je Sheet Mask ni nini?
Jina lenyewe linaweza kuwa jibu tosha, sheet mask ni kipande cha nguo ambacho kina umbo la sura/ uso,kipande hiki kimewekwa viungo mbalimbali vya kutunza ngozi kama vitamin, minerals, hyaluronic acids, collagen, and antioxidants.
Sheet hii imetengenezwa kwa materials mbalimbali kama fiber,cotton, cellulose, or coconut pulp. Kama mask nyingine sheet mask pia ina vitobo kwenye macho, puani na mdomoni kukusaidia kwenye kuona, upumuaji na kuongea lakini sehemu nyingine zote imefunikwa.
- Sheet Mask Ina Faida Gani?
Sheet mask ni njia ya haraka yenye ufanisi ambayo husaidia kurudisha mng’ao na ung’avu wa ngozi yako, faida kubwa ya sheet mask ni kwamba inashikamana na ngozi yako kama ngozi ya pili na kusaidia viungo vya kutunza ngozi vilivyowekwa kwenye mask hii kuingia vyema kwenye ngozi yako ya uso.
Facial mask zimeloekwa katika high potency serum ambazo husaidia kutatua matatizo ya ngozi mbalimbali kutokana na hitaji lako mfano,ukavu wa ngozi, chunusi,madoa meusi na ngozi iliyofifia ( dull skin).

Zina viambatanisho vya kung’aza ngozi yako kama vile vitamin C,niacinamide, licorice, and mandelic acid ambazo husaidia kuipa ngozi yako iliyochoka maisha/muonekano mpya, kufanya ngozi yako kuwa na rangi moja pamoja na kung’aza ngozi iliyofifia.
Kwa upande mwingine sheet mask ina viungo kama tes tree oil, aloe vera oil,n tea, algae, and salicylic acid ambazo husaidia kusafisha vinyweleo, kuondoa uchafu katika ngozi,kuzuia break outs pamoja na kupunguza uvimbe unaotokana na chunusi.
- Unaitumiaje Sheet Mask?
Baada ya kuosha uso wako na kufanya toning weka sheet mask yako kwa dakika 15-20 unaweza kuiacha na usioshe baada ya kuitoa,haina madhara na itakusaidia kutunza ngozi yako hata baada ya kuitoa.
Hakikisha unaiacha kwa muda unaotakiwa nauitoe usiache kwa muda mrefu inaweza kusababisha madhara kama kuiacha ngozi kuwa kavu zaidi.
- Je Ni Sawa Kuosha Baada Ya Kutoa Sheet Mask?
Ni vyema usipoosha inafanya viungo vizidi kuingia kwenye ngozi cha muhimu ni ku-pat ngozi yako na kufanya vilivyokuwepo kwenye sheet mask kuzidi kuingia kwenye ngozi na kukupa matokeo mazuri zaidi.
- Upake Nini Mara Baada Ya Kutumia Sheet Mask?
Unaweza kupaka mafuta au kuendelea na skincare routine yako ya kawaida kama kupaka moisturizer, sunscreen, eye cream au night cream.
- Muda Gani Na Mara Ngapi Utumie Sheet Mask?
Sheet mask zinaweza kutumiwa mara nyingi uwezavyo ila muda mzuri zaidi ni asubuhi na jioni, na unaweza kuzitumia kila siku, mara kwa moja kwa week,inategemea na tatizo lako na namna umeelekezwa kutumia sheet mask yako.
- Unahifadhi Vipi Sheet Mask?
Sheet mask inatakiwa ihifadhiwe kwenye room temperature hakikisha huiweki kwenye jua, na kama utaamua kuihifadhi kwenye fridge ni vyema zaidi.
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…