SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Shekha Manjano Ametueleza Jinsi Gani Ameweza Kubaki Imara Katika Soko La Bidhaa Za Urembo
One on One

Shekha Manjano Ametueleza Jinsi Gani Ameweza Kubaki Imara Katika Soko La Bidhaa Za Urembo 

Kama kuna bidhaa ya kipodozi Tanzania ambayo imekuwa ikiendelea kuwepo katika soko toka ianzishwe imeweza ku-remain constanty basi ni hii shear Illusions ambayo ndani yake kuna kampuni ya vipodozi ya Luv Touch Manjano, Kutokana na wimbi la watu maarufu kuanzisha bidhaaa mbalimbali na urembo na kushindwa kuendelea imebidi tumtafute da Shekha na kujua zaidi ni vipi ameweza na ana washauri nini wanaoanza

Afroswagga : Tunamjua Shekha Kidogo Sana Lakini Tunajua Kuhusu Shear Illusions Pia, Tungependa Kujua Machache Ambayo Hatuyajui Kuhusu Shekha Ni Nani Na Kwanini Akaamua Kufanya Urembo? Na Shear Illusions Ilitokana na Nini?
Shekha Manjano : Mimi nimezaliwa Tabora kwenye familia ya kawaida nimekulia mjini na kijijini pia na wala sikuwa na ndoto kwamba siku moja naweza kuwa mtu mwenye mafanikio na kuwa role model wa wengi. Alhamdulillah. Shear illusions nilianzisha baada ya kuwa kwenye ajira katika mikataba ya muda wa miaka 15 sikuwa na full-time employment bali nilikuwa nikihamishwa kutoka mradi mmoja kwenda mwingine. Mradi ulikuwa ukiisha nakaa nyumbani mwezi au hata minne bila kuwa na mshahara. Hapo ndipo nikaona ni bora kuanzisha biashara ili hata kama mradi utakwisha nisihangaike kutafuta ajira tena bali niwe na kipato cha kunikimu mahitaji yangu muhimu ambayo ni chakula, mavazi na malazi. Niichagua biashara ya urembo sababu niliamini ni biashara nitakayoifanya muda mrefu sababu urembo ulikuwepo kabla sijazaliwa na biashara ya urembo na vipodozi itaendelea kuwepo mpaka siku naiacha dunia.
Afroswagga : Je, ni mambo gani muhimu zaidi uliyoyazingatia wakati wa kujenga Shear Illusions?
Shekha Manjano : Mambo niliyozingatia ni pale nilipopata elimu ya biashara nikasoma case studies (yaani historia za tafiti ya makampuni mbali mbali) za makampuni yaliyodumu hata baada ya vita kuu vya dunia. Mambo muhimu ya kuzingatia ni manne; ni kujali mteja (customer care), kutangaza biashara mara kwa mara, kutengeneza bidhaa bora (quality) na za kudumu na mwisho ni kuwa biashara iwe inasaidiaje watu (is it useful).
AfroswaggaShear Illusions Ime wezaje Ku Maintain Status Yake Mpaka Sasa? Kwa Sababu Wengi Wanajaribu Kuinvest Katika Bidhaa Za Urembo Na Wanaishia Njiani Je Kwako Wewe Umewezaje?
Shekha Manjano : Nadhani ni kwa sababu ya nidhamu. Mimi nafuata ueledi katika kazi zangu zote, pesa ya mauzo yote yanapelekwa benki, sishiki hata mia moja itokanayo na mauzo ya madukani. Siruhusiwi kushika au kuchukua pesa kwenye account bila idhini ya muhasibu na lazima pesa itoke kwenye budget iliyopitishwa. Kila mwisho wa mwezi ni lazima mishahara, kodi na suppliers walipwe hata kama tutakuwa na ukata kiasi gani. Wengi hufeli sababu pesa za mauzo huzitumia vibaya na bila control ya cash flow unakuwa hujui mapato yako kwa mwezi na bila kuweka kumbukumbu za biashara ni vigumu kujua matumizi yako kwa mwezi na kujitathmini wapi ba kubana matumizi na wapi pa kulipa na nani asubiri. Wakati mwingine nadhani kumweka Mungu mbele inasaidia kuwa humble na kutokufanya mambo kwa kufurahisha watu bila kujali kipato chako.
Aforswagga : Tukiongelea Kuhusu Soko La Kimataifa, Watu Maarufu Mbalimbali Wanaonekana Kuvutiwa Na Soko Hili Na Kuanzisha Bidhaa Zao Je Umejiandaaje Na Competition?
Shekha Manjano : Bado bidhaa za LuvTouch Manjano ni changa. Tumezindua nchini mwaka 2015 na mpaka sasa tuna re-sellers 360 nchi nzima. Tungependa kuwa na resellers zaidi kwanza Tanzania kabla ya kuingia soko la kimataifa. Ushindani upo isipokuwa bidhaa zangu zina Quality ya hali ya juu sana na bei yake ni ndogo sana ukilinganisha na bidhaa za nje. Mfano poda ya LuvTouch Manjano hudumu kwa saa 12, na hata ukitokwa jasho haichuruziki. Bidhaa yenye ubora huu kutoka nje bei yake ni kuanzia TSh.125,000 mpaka TSh.160,000 wakati poda yetu huenda kwa TSh.30,000 tu. Makeup artists wengi wanajua ninachoelezea kuhusu quality products katika vipodozi vya makeup.
Afroswagga : Watu Wengi Hasa Wenye Dark Skin Wamekuwa Wakilalamikia Kukosa Vipodozi Vyenye Kuendana Na Rangi Zao Katika Brand Mbalimbali Za Urembo Je Shear Illusions Ina Provide Vipodozi Vya Watu Wenye Dark Skin? Kama Hapana Wavitegemee Kuanzia Lini?
Shekha Manjano : Shear illusions imeleta sokoni bidhaa za LuvTouch na zipo rangi za kila mmoja kuanzi mtu mweupe mpaka mweusi. Watu wa rangi zote hupata rangi ya kuendana na ngozi zao. Hivi karibuni tutaleta foundation ya maji ya LuvTouch Manjano ambazo hufaa sana kwa ngozi kuu (mature skin).
Afroswgga : Je Ni Kipodozi Chako Kipi Ndio Pendwa Zaidi Katika Brand Yako
Shekha Manjano : LuvTouch Manjano #KipodoziPendwaTanzania
Afroswagga : Kama Owner Wa Kampuni Ya Vipodozi Tunajua Moja Kwa Moja Unapenda Urembo Unaweza Kutupa Tips Chache Za Kujali Ngozi Yako?
Shekha Manjano : Asante. Tips za kutunza ngozi kwanza mlengwa afahamu kuwa ngozi yako ya sasa ndio utakayoirithi ukifika uzeeni. HIvyo huna budi kuitunza sasa.
– Soma au tembelea wataalam wa ngozi kujua namna ya kutunza ngozi yako
– Epuka kutumia mikorogo au bidha za zenye kemikali zinazodhuru ngozi,
– Sahani yako ya mlo iwe na rangi kama ya Rainbow.. majani, matunda na vyakula vinavyo jenga. Achana na vyakula vinavyo haribu ngozi mfano vitu vyenye mafuta mengi, sukari na chumvi nyingi.
– Avoid kukaa kwenye jua kali muda mrefu au kupika kwenye moto mkali huku uso wako uko karibu na moto.
– Hakikisha unakunywa maji mengi at least glasi nane kwa kutwa nzima kuanzia unapoamka mpaka unapoenda kulala hesabu kuwa umekunywa JUMLA glasi nane za maji. Maji ni dawa sana sio tu kwa afya yako, kusaidia kulainisha choo (digestion) lakini kikubwa seli ya ngozi (skin cells) hujengwa kwa asilimia kubwa na maji.
–  Tumia bidhaa natural kupaka kwenye ngozi yako, mfano mafuta ya nazi, mwani, aloe vera, manjano, nk.
– Jitahidi mara moja kwa mwezi kufanya scrub na facial ya uso wako kutumia natural products kama mwani, manjano au ndimu na asali
Afroswagga : Wakati wa utengenezaji wa Vipodozi huwa mnaangalia na skin types za watu? Na kama ndio ni namna gani watu wanaweza kutambua kipodozi hiki cha Manjano Kinamfaa na hiki hakimfai?
Shekha Manjano : Aina za ngozi kuu ni ngozi ya mafuta na ngozi kavu. Pale mtu ananunua bidhaa ya kupaka usoni iiyoandikwa “For Dry Skin” na wakati ana uso wa mafuta lazima atapata madhara usoni sababu anajiongezea mafuta zaidi usoni kwa kutumia bidhaa zilizotengenezwa kwa watu wenye ngozi kavu. Na mtu anaponunua bidhaa zilizoandikwa “For Oily Skin” wakati ngozi yake ni kavu basi hawezi pata muonekano wa kuvutia sababu anatumia bidhaa za kukausha mafuta usoni kwake wakati tayari yeye uso wake mkavu sababu ametumia bidhaa mahsusi kwa watu wenye ngozi za mafuta. Ndio maana bora utumie natural products. Mfano mtu mwenye ngozi ya mafuta atatumia manjano, asali na ndimu au mwani kupunguza mafuta usoni. Na mtu mwenye ngozi kavu atatumia parachichi na manjano kulanisha ngozi yake iwe na moisture. Bidhaa za Manjano huuzwa na wataalam wanaoweza kutoa ushauri na kutambua aina ya ngozi ya mteja.
Afroswagga :  Tips chache kwa wajasiriamali ambao wangependa kuinvest katika vipodozi na hawajui waanzie wapi.
Shekha Manjano : Anza kidogo na mwisho utakua. Mfano kuna bidhaa nyingi za asili za kutunza na kulinda ngozi ambazo bibi zetu walikuwa wanazitumia enzi na anzi. Ni vyema kufanyia kazi hizo bidhaa na kuziweka katika vifungashio vizuri vya kisasa ili kuongeza thamani. Mfano kuna dada mmoja nchini Nigeria aliyechukua sabuni ya asili iliyokuwa maarufu nchini kwao Nigeria inayoitwa Dudu Osun. Sabuni hii ni nyeusi kwa rangi lakini ni nzuri sana kwa kutunza ngozi. Aliweza kuanza na mtaji wa dola 100 tu na kuzi package nyumbani kwake kwa kutumia bidhaa za asili na kuziuza ndani na nje ya nchi. Kwa hivi sasa brand yake ni global brand inayopendwa na wazungu kwa waafrica na watu wenye ngozi za aina zote, wahinidi, wachina nakadhalika. Hakuanzia na mtaji mkubwa na hivi sasa ni billionnaire. Sabuni yake inatengenezwa kwa mkono kwa kuchanganywa entirely from natural ingredients mfano asali, shea butter, mafuta ya mawese na aloe vera yaani mzaituni. Kilichomfanya afanikiwe ni nidhamu na kutokutia tembo maji, wengi wajasiriliamali wakishakuwa na kupata order nyingi wanaharibu biashara kwa kulipua hivyo kuwakimbiza wateja hatimae biashara inakufa.
Afroswagga : Tutegemee nini kutoka katika Shear illusions hivi karibuni na chochote
Shekha Manjano : Hivi karibuni natarajia kuleta perfumes, wanja, eyeshadow, mascara na liquid foundation zote bidhaa bora za LuvTouch. Bidhaa zote zitakuwa nzuri katika viwango vya kimarekani. Bila shaka nitakupa for testing and product reviews na followers wako.
Asante.

Related posts

2 Comments

  1. 週刊 エステ

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/shekha-manjano-ametueleza-jinsi-gani-ameweza-kubaki-imara-katika-soko-la-bidhaa-za-urembo/ […]

  2. shroom chocolate bar Michigan

    … [Trackback]

    […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/shekha-manjano-ametueleza-jinsi-gani-ameweza-kubaki-imara-katika-soko-la-bidhaa-za-urembo/ […]

Comments are closed.